ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 1, 2014

TFF yashauriwa kumtembeza Mart Nooij mikoani.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetakiwa kumtembeza Kocha wao wa Taifa, Mart Nooij mikoani, ili afahamiane na wadau sanjari na
kutambua vipaji vilivyopo Tanzania.
Katibu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela, alitoa wito huo hivi karibuni, alipozungumzia juu ya ujio wa kocha huyo.
“TFF wanapaswa waangalie namna ya kocha wao kufanya ziara mikoani na sio kukaa ofisini tu au kusubiri mechi kubwa.
“Hapo itamuongezea ari kubwa ya kufundisha na kuwa mkali kwa kile anachowaelekeza wachezaji wake,” alisema.
Kwa mujibu wa Mwakalebela, wakati yupo TFF walifanya hivyo kwa kumtembeza aliyekuwa kocha wao, Mbrazil, Marcio Maximo.

No comments: