01 – 06 - 2014
TATHMINI KUHUSU UFINYU WA BAJETI INAYOTENGWA KWA AJILI YA DAWA MUHIMU, VIFAA TIBA NA VITENDANISHI
Ukosefu wa mara kwa mara wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya huduma za afya vya umma bado ni tatizo Tanzania. Tatizo hili linachangia kutolewa kwa huduma duni za afya zinazopelekea athari kwa afya za wananchi. Tathmini mbalimbali zimeonesha kuwa upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba ni mdogo katika vituo vya huduma za afya vya umma. Kwa mfano, utafiti uliofanywa na Sikika mwaka 2012 umeonesha kuwa asilimia 52 ya hospitali [N=52] hazikuwa na dawa muhimu na vifaa tiba kwa zaidi ya wiki nne. Moja yasababu kuu za kukosekana kwa dawa muhimu na vifaa tiba ni bajeti ndogo inayotengwa na serikali.
Mwenendo wa mgao wa fedha za dawa muhimu na vifaa tiba kutoka Bajeti ya WAUJ kutoka 2008/09 hadi 2014/15
Chanzo: Sikika 2010/2011 Health Sector Budget Analysis, Sikika Budget Analysis of the MoHSW for fiscal year 2013/14. |
Mahitaji ya dawa muhimu na vifaa tiba Ingawa mojawapo ya vipaumbele vya
Wizara ya Afya ni kuboresha upatikanaji wa dawa muhimu, mgao wa fedha
kwa dawa muhimu na vifaa tiba umekuwa hauendani na mahitaji yake. Kwa
mfano kwa mujibu wa makadirio ya Wizara ya Afya zitahitajika kiasi cha
Tsh 250 bilioni kukidhi mahitaji ya dawa muhimu kwa mwaka wa fedha
2014/15. Hata hivyo, mgao unaotarajiwa kupangwa ni shilingi bilioni 45
tu. Mgao huu ni sawa na asilimia 7.7 ya mahitaji.
Pamoja na hivyo, ingawa kipaumbele cha Wizara ya Afya ni kupungunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na kujifungua, bajeti ya vifaa vya kujifungulia (delivery kits) inapungua mwaka hadi mwaka. Mfano, kwa mwaka wa fedha 2012/13 zilitengwa jumla ya Tsh bilioni nne kwa ajili ya vifaa vya kujifungulia.
Bajeti hii ilipungua kufikia bilioni tatu mwaka 2013/14, na kama hakutakuwepo mabadiliko itapungua hadi kufikia shilingi bilioni moja na nusu mwaka ujao wa fedha 2014/15. Pia, pamoja na serikali kuahidi bunge mwaka jana kulipa deni ambalo MSD inaidai serikali, deni hilo limeongezeka toka shilingi bilioni 76 mwaka 2013 hadi bilioni 89 mwaka 2014
Mjadala wa Bunge juu ya Bajeti ya WAUJ
Mapitio ya hansards (2008/09 – 2012/13) yamebaini kuwa takribani
asilimia 35 ya wabunge ambao huchangia katika mjadala wa bajeti ya Afya
hulalamika kuhusu uhaba wa dawa vituoni na huitaka serikali, pamoja na
mambo mengine kuongeza bajeti. Tunawapongeza Wabunge kwa kazi hii nzuri.
Lakini kama
ilivyoainishwa hapo juu, bajeti ya dawa imekuwa ikipungua na uhaba wa dawa muhimu umeendelea kuwepo. Pia akina mama wanaojifungua wameendelea kulalamika ukosefu wa vifaa vya kujifungulia
ilivyoainishwa hapo juu, bajeti ya dawa imekuwa ikipungua na uhaba wa dawa muhimu umeendelea kuwepo. Pia akina mama wanaojifungua wameendelea kulalamika ukosefu wa vifaa vya kujifungulia
Mapendekezo
- Serikali itafute fedha za ziada kutoka katika sekta nyingine (kuhamisha) ili kuongeza bajeti ya dawa muhimu inayotarajiwa kutengwa kwa mwaka wa fedha 2014/15 kutoka bilioni 45 hadi bilioni 250 (kwa mujibu wa makadirio ya Wizara ya Afya)
- Wizara ya Afya na ustawi wa Jamii ihamishe fedha kutoka kwenye idara nyingine kwenda kwenye dawa muhimu na vifaa tiba ili kuweza kuwa na bajeti inayolingana na mahitaji.
- Serikali ijadiliane na wafadhili ili waweze kuongeza fedha katika bajeti hii ya mwaka 2014/15 (kama suluhisho la muda mfupi) wakati ikiendelea kubainisha suluhisho la kudumu kama kuboresha na kusimamia ukusanyaji wa kodi, kupunguza au kuondoa misamaha ya kodi pia kuboresha makusanyo yannayokana na mifuko ya afya kama Mfuko wa Afya wa jamii(CHF) na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa.(NHIF). Serikali inapaswa kuwa Mchangiaji mkuu wa dawa muhimu na vifaa tiba na sio kuwaachia jukumu hili wafadhili.
- Mipango na mgao wa bajeti unapaswa kuzingatia mapendekezo yaliyotolewa na bunge kupitia kamati ya kudumu ya huduma za jamii.
Mr. Irenei Kiria
Executive Director of Sikika, P.O. Box 12183 Dar es Salaam,
Tel: +255 222 666355/57, Fax: 2668015, Email: info@sikika.or.tz, Website:
No comments:
Post a Comment