ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 1, 2014

Mbwembwe Malawi -Rais Mpya kushika doria


Mutharika kuapishwa kama rais mpya malawi
Viongozi wa Mataifa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria sherehe za kumkabidhi madaraka rais mpya wa Jamhuri ya Malawi hii leo.
Rais mpya Profesa Peter Mutharika atachukua rasmi uongozi wa nchi hiyo baada ya kushinda uchaguzi mkuu. Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre kuwa serikali imetoa mwaliko kwa wakuu wa nchi kadhaa za Afrika wakiwemo majirani zake wote ili kushuhudia hafla hiyo muhimu.
Shughuli hiyo itafanyika kwenye uwanja wa Taifa wa Kamuzu uliopo jijini Blantyre ambapo Bw. Mutharika atapokea mamlaka ya juu ya nchi hiyo kutoka kwa Dr Joyce Hilda Banda ambaye ameongoza Malawi kwa miaka 2 iliyopita ikiwa
ni baada ya kufariki kwa Rais Bingu wa Mutharika.
Jumamosi asubuhi Jaji mkuu Anastazia Msosa alimwapisha Mutharika kuwa Rais wa tano wa Malawi ikiwa ni saa 12 tu baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliokuwa umejaa malalamiko ya wizi wa kura na pingamizi mahakamani.
Akizungumza nyumbani kwake baada ya kula kiapo, Rais Mutharika amewaahidi wamalawi uhudumu bora na kumaliza kiu yao ya maendeleo, huku akiwataka wapinzani wake katika mbio za urais akiwemo Dr Joyce Banda waungane naye kuijenga Malawi.
Dr Banda pamoja na wagombea urais wengine 11 walioshindwa, wamempongeza Rais mpya na kuwataka wafuasi wao kukubali matokeo na kujipanga upya kwa uchaguzi ujao wa mwaka 2019

No comments: