Advertisements

Tuesday, June 10, 2014

MAJINA YA WAGOMBEA UONGOZI JUMUIYA YA WATANZANIA DMV HAYA HAPA

KAMATI MAALUM YA UCHAGUZI- DMV

TANGAZO RASMI:
MAJINA YA WAGOMBEA UONGOZI KATIKA JUMUIYA YA WATANZANIA DMV 2014.

RAIS:                                                                  MAKAMU WA RAIS:
1.     IDDY SANDALY                                       1. HARIETT SHANGARAI
2.     LIBERATUS MWANG’OMBE               2. SALIMA SULEIMAN

KATIBU:                                                            MAKAMU WA KATIBU:
1.     SAID MWAMENDE                                1. SOLOMON CRIS
2.     ISMAIL MWILIMA

MWEKA HAZINA                                             MAKAMU WA MWEKA HAZINA
1.     JASMINE RUBAMA                               1. JACOB KINYEMI



Kamati ya Uchaguzi wa viongozi wa Jumuia ya Watanzania- Washington Metro (ATC), inawatangazia kuwa uchaguzi ufanyika JULY 20, 2014 kuanzia saa saba mchana hadi saa kumi na mbili, anuani ya ukumbi utatangazwa baadaye.
Taratibu zitakuwa kama zifuatazo:

1.     JUNE 19, 2014 ni tarehe ya mwisho kupokea malipo ya ada kwa wale watakaoshiriki kupiga kura; kwa mujibu wa katiba kila mpiga kura au mgombea wa uongozi wa Jumuiya lazima wawe wanachama hai kwa siku zisizopungua thelathini.
2.     Hakuna malipo yeyote yatakayopokewa mlangoni siku hiyo ya kupiga kura.
3.     Ukitaka kulipia ada yako tembelele tovuti ya jumuiya utapata maelezo au tutumie barua pepe uchaguzi2014@gmail.com na tutakusadia kulipia ada yako na kuwa na haki ya kupiga kura.
4.     Kama ulilipia kwa mwezi mmoja kumbuka kulipia mara ifikapo tarehe hiyo mwezi unaofuata,mfano kama ulijiunga au kuongeza muda wako June 6, 2014 uanachama wako unakoma siku July 6, 2014, ili uweze kupiga kura July 20, 2014 itakubidi ufanye malipo mengine ya ada ($10) kabla ya July 6, 2014.
5.     Kamati inawatangaza rasmi wagombea hapo juu na wagombea wanaweza kuanza kampeni kuanzia June 10, 2014.

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu,

Kamati maalum ya Uchaguzi DMV 2014. 

15 comments:

Anonymous said...

Haya tena ni kipindi kigumu kimefika kwa wana DMV kutafakari ni nani atuongoze. naamini kuwa kila mgombea anafaa kuongoza ila tu nafasi ni moja.na atakaye shindwa akubali matokeo na atoe ushirikiano kwa mshindi.

Anonymous said...

Raisi wangu mpya ni Libe

Anonymous said...

Raisi wangu mpya ni Libe

Anonymous said...

Rais wangu ni Iddi

Anonymous said...

Libe hafai kabisa kuwaongoza Wananchi CHADEMA yenye itikadi moj inamshina chama kisha dolola wamebakia na wanachama 5 DMV Libe hajawahi kuitumikia jumuia zaidi ya kucheza mpira ni kiongozi aiyeamini Mungu atawezaje Jumuiya yenye watu na iman zao za dini? mijumuisho mingi sana ishatokea hapa DMV lakini libe hupendelea zaidi kwenda kwenye mijumuiko ya starehe na kamwe hutamuona kwenye mijumuiko ya misiba na mambo mengine ya kusaidiana. Libe hafai hafai kua kiongozi ni mtu anayeleta migawanyiko kwenye Jumuiya. Libe is not a good leader . My Advise Libe don't waste your time you will regrate big time on this DMV haukuzimi na hapa sio sehemu ya kuufanyia mazoezi Ubunge wako. Libe umekaa Kichadema zaidi kuliko Kijumuiya asante.

Anonymous said...

Libe for President

Anonymous said...

Libe for president and I approve this massage. Libe ingawa ni CHADEMA inaonesha wazi ni mtetea haki la sivo angekuwa CCM kwenye kujaza matumbo. Libe uwa anatuelimisha sana Facebook na updates za Tanzania he spends most of his time educating us he is A TRUE LEADER. Sio Yule wakuzengea shuguri ili uwe mtu wa watu wakati watu wenyewe uwasaidii hata kimawazo. Amashasaidia sana vijijini bongo anapiga vita mafisadi 25/7 HE IS A TRUE LEADER Kama hamumuoni kwenye mapilau na maubwawa ni kwa ajiri anakuwaga busy kuijenga Tanzania nzima itakuwa hicho ki DMV?????? Atashinda tena kwa kishindo ki kubwa sana.

Anonymous said...

Kwanza idd sandaly nae anapendelea CCM wakati waheshimiwa wakija kutoka bongo huwa tunamwona yeye na viongozi wa CCM mbona viongozi wa CHADEMA hawaalikwi Mfano picture zinazofuatia za waziri wa madini Yuko yeye na CCM. Pia ameshakutana na viongozi Wengi mbona hafanyi nao debate itakayo tusaidia sisi wa ughaibuni yeye ni kula kula misosi ubalozini tu!. ONLY LIBE CAN CHALLEGE OUR CORRUPTED LEADERS WHO VISIT USA. Sandaly haiwezi hiyo kazi. ( DJ usiminye comment )

Anonymous said...

Rais wetu ni Iddi Sandaly

Anonymous said...

Huyo Libe anadhani akiwadhalilisha viongozi ndio anapata umaarufu!! Hapati kura yangu ng`oo!!! Upinzani ni kuwa na busara na kujenga hoja,sio jazba na dharau kwa serikali ambayo imechaguliwa na majority. Wether u r cuf,ccm,chadomo wote tunawajibu wa kuheshimu matokeo na viongozi. So NOOO LIBE!!!! PLEASE!!!!

Anonymous said...

Hapo tuuuu DMV

Anonymous said...

Annonimous wa 2:36 pm. Kwa taharifa yako CCM haikuchaguriwa na Majority. Asilimia ndogo sana ilichaguwa CCM . Chunguza utapata jibu. Na kueleza ukweli viongozi sio kuwadharirisha wewe bado uko kwenye Karne ya zamani sana enzi za watoto walivokuwa hawana SAY SO. Sikuhizi watoto wanaeleza wazazi zao ukweli wa makosa Yao. Kalaga bao ndo mana rasilimali midhaabu na halmasi ...mpaka wanyama wanatoroshwa mnakaa kimya eti kisa mkiwaeleza mtawakose Adabu viongozi pole sana.

Anonymous said...

IDD SANDALY MZEE NA MDA WAKE UMEPITA WAZEE WOTE WAONDOKE WAPISHE VIJANA - MAHAGIZO YA MWESHIMIWA WARIOBA..

Eti chadomo mngekuwa wapi Leo Kama sio CHADEMA. Hata Zanzibar haiko huru inatawaliwa na CCM muishukuru chadema/CHADOMO Imewakomboa watanzania.

Anonymous said...

Watu wa DMV wengi wako smart,tunasuburi siku ya kura tumchague kiongozi mwenye uelekeo,sifa,hekima,mpenda watu ktk shida na raha,anaejitoa kwa hali na mali,si mwingine ni kaka yetu mpendwa,IDDI SANDALY!! Bro,sikujui ila kwa vitendo vyako vya kibinadamu,nafsi yangu itanisuta kama nitakupinga,ubarikiwe sana

Anonymous said...

Tatizo itachukua loong time kukuelimisha,in short,mfano,DMV wabongo wako mamia,wanachama hai ni less than 100,na ndio wanaoruhusiwa kupiga kura. Ni jukumu la kila mtu kujiandikisha,ila wazembe wengi,akishachaguliwa kiongozi,mnabaki kulialia! Nani kakuzuia kutumia right yako to vote,noone than ur own laziness!! So GET OVER IT!!!!! KIKWETE IS A LEGIT PRESIDENT,KNOWN IN TANZANIA& ALL OVER THE WORLD!!!! Go to school is my advice