Wazee katika baadhi ya nchi
huheshimika na kuwa akiba ya busara kwa kizazi cha vijana na zaidi ya
yote huangaliwa na kusaidiwa kimaisha.
Huko nchini Korea Kusini maisha kwa wazee ambao
walichangia katika uchumi wa taifa hilo na ustawi wa taifa hivi sasa
wanaishi katika mazingira magumu hali ambayo kwa wanawake wazee
inawalazimu kubuni mbinu mpya za maisha kwa kujitumbukiza katika
biashara haramu ya ngono kwa kuuza miili yao ili waweze kujipatia fedha
za kuendesha maisha yao ya kila siku.ngono hufanywa na wasichana wadogo.
Akiwa amevalia koti lake jekundu,na kupaka rangi ya mdomo kwa ustadi Bi. Kim Uen Ja mwenye umri wa miaka 71 mavazi yake yanabainisha wazi kwamba angependa kuwa na muonekano wa msichana mdogo na mrembo, yupo katika eneo la kupumnzika la Jongno-3 subway station huku pembeni mwake akiwa na begi kubwa lililosheheni chupa ndani yake.
Bi. Kim ni mmoja kati ya wanawake wazee wa Korea ya kusini ambao hupendelewa kuuza kinywaji ambacho wanaume wanasema kinawaongezea nguvu kijulikanacho kwa jina la Bacchus, lakini wanawake hawa wanaouza vinywaji hivi baadhi yao ni wale wenye malengo ya kujiuza ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.
'Siwezi kuwategemea watoto wangu kunisaidia katika maisha, kwa sababu wapo katika matatizo kwani wanapaswa kuanza kujiandaa kukabiliana na maisha yao ya siku za uzee wao,anasema Bi.Kim.
"Unaona wanawake wote waliosimama pale?anauliza, wote hao wana biashara nyingine zaidi ya kinywaji hiki Bacchus, kuna wakati wanakwenda na wazee hao wakiwa wamewanunua kimapenzi na wanajipatia fedha nyingi toka kwao,japo mimi siishi kama wao anawabeza.
Mwanamke huyu mzee akielezea mapato yake anasema hupata hadi dola tano kwa siku ama paundi tatu,kwa kuuza kinywaji chake kwa mfumo wa haraka haraka mwenyewe akiuita 'drink up fast.'
''Polisi muda wote hunishangaa ninavyofanya kazi zangu,'' anasisitiza mwanamke huyu.
''Sisi ni wanaume bwana na tunapenda wanawake,tunapata kinywaji,kiasi kingine cha fedha tunawapa hawa wanawake kwaajili ya kuwapata kimapenzi, kisha akacheka kidogo na kumalizia kwa kusema na kwa hakika tunawapata, na kwetu haijalishi ati ni wazee sana ama hawana msisimko wa kimapenzi hilo si tatizo''alisema mwanaume mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 60.
"Tunaweza kupata marafiki wa kike hapa si unawaona wale wanawake waliosimama pale? Wapo pale wakihitaji tuwalipe kasha twende nao,gharama ya kuwapata ni kati ya paundi 11 hadi 17 lakini wakati Fulani kunakuwa na punguzo wanakubali tu''anasema mwanaume mwingine mwenye miaka 81 hivi.
'Nina hasira, tena hasira kali, sihitaji heshima yoyote, ninachohitaji ni kupata chakula mara tatu kwa siku'anasema mwanamke mzee anayejiuza.
Serikali inafanya jitihada kukomesha hali hiyo japo kuwa raia hao hawana akiba ya fedha,bima ya maisha ama malipo kwaajili ya kuwasaidia wazee hali inayowafanya kushindwa kujitegemea.
Polisi ambao wamekuwa wakiendesha doria kuwasaka wanawake hao wanaojiuza wanasema tatizo hili ni kubwa na kwamba hawadhani kama linaweza kukomeshwa kkwa urahisi ati kwa kuwaweka chini ya ulinzi bali sera kwa ujumla inapaswa kubadilika.
Hata hivyo kwa wale wanaobainika na kupekuliwa katika mabegi yao wanakutwa na sindano ambazo wanawake hao huwadunga wanaume kwenye mishipa ili kusisimua kwa wanaume hao wazee ambao wengi wao hawana nguvu za kimapenzi hali ambayo imesababisha asilimia 40 kukutwa na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na kujamiana.
BBC
No comments:
Post a Comment