MAKUBWA! RB nambari TBT/RB/3478/2014 ya Kituo cha Polisi Tabata, jijini Dar es Salaam ina kesi ya dereva taksi aliyepatikana kwa jina moja la Lindoya akidaiwa kuharibu mali za Asia Hakika kwa sababu eti alinyimwa unyumba, Uwazi linakuhabarisha.
Asia Hakika anayedai kuharibiwa mali zake na dereva taksi aitwaye Lindoya.
Mlalamikaji
Asia, mkazi wa Tabata – Chama na mtuhumiwa Lindoya mwenye makazi yake
Mbezi – Makabe ni wapenzi wa muda mrefu sasa, lakini baada ya Asia
kugundua kuwa mwenzake ana mke na watoto, akagoma kumpa tendo la ndoa,
jambo lililoibua kisanga hicho.
Akizungumza
na Uwazi, Asia alisema: “Lindoya ni mpenzi wangu, tulikuwa tunaelekea
kuwa mume na mke, maana tumeishi kwa miaka miwili sasa, lakini siku zote
amenieleza kuwa hana mke wala watoto, lakini nimegundua kuwa
alinidanganya.
Asia Hakika akiangalia mali zake zilizoharibiwa.
“Ana
mke na watoto wawili, nikaamua nimuache aendelee na familia yake.
Akakataa, anataka kunitumia tu. Nilipomkatalia ndiyo akaamua kuniharibia
vitu vyangu. Alinikuta nina vitu vya ndani nilivyonunua kwa fedha
zangu, nimepanga chumba kwa pesa yangu na aliniomba tuishi pamoja
nikamkubalia.
“Baadaye
akaanza kujenga nyumba huko Mbezi ya Makabe, nilifurahi sana niliamini
kuwa tukioana tutakua tunaishi huko lakini cha kushangaza baada ya
kumaliza kujenga alimfuata mkewe huko Mbeya, wakahamia na watoto wake.”
Alisema,
mpenzi wake huyo zilipendwa, alimwambia asikanyage nyumbani kwake kwa
kuwa mkewe amekuja, jambo ambalo alikubaliana nalo kwa sharti kuwa
wasitishe uhusiano wao lakini Lindoya akaonekana kutoridhika.
Baadhi ya mali za Asia Hakika zilizoharibiwa.
“Siku
moja nikiwa kazini, alifika nyumbani kwangu akafungua mlango kwa funguo
wake, maana kila mmoja alikuwa na wake; akaharibu mali zote ndani,
akaacha kitanda tu. Nimeumia sana kwa kweli,” alisema Asia.
Kwa
sasa kesi hiyo ipo katika Kituo cha Polisi Tabata kwa uchunguzi ambapo
jalada la uchunguzi limeandikishwa kwa namba TBT/IR/2032/2014.
GPL
3 comments:
We dada ungetoa unyumba ungekuwa relaxed na pia unge-enjoy kuliko jinsi sasa hivi ulivyo so confused and frustrated kwa kwenda mahakani wakati unajua TZ hakuna sharia. Just give it up!
We anonymous wa mwanzo.
Nadhani ama una ugonjwa wa akili au umelewa.
Anon wa mwanzo, uko sawa wewe kweli?
Utakuwa umevuta yale majani makavu. Subiri handas ishuke ndio ulete comments zenye busara.
Post a Comment