ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 20, 2014

Marekani yaiadhibu Uganda kwa Kupinga Ushoga

Marekani imeadhidhibu Uganda kwa kuweka sheria kali ya kupinga mapenzi ya jinsi moja katika taifa hilo.
UGANDAMsemaji wa Whitehouse, Caltlin Hayden ameeleza katika barua yake kwa
vyombo vya habari kuwa sheria iliyopitishwa na bunge la Uganda ikiuka haki za binadamu.
Vikwazo vya Marekani kwa Uganda kama adhabu, vinajumisha kuwapiga marufuku wanaharakati waliopigia debe sheria hiyo kutoingia Marekani.
Marekani itapunguza ushirikiano na Wizara ya Polisi na Afya za Uganda, na kuachana na mpango wa mazoezi ya kijeshi kati ya wanajeshi wa Marekani na wanajeshi wa Uganda.
Uganda walipitisha sheria ambayo inaeleza wazi mtu atakayekutwa na hatia ya kushiriki katika masuala ya ushoga atahukumiwa kifungo cha maisha jela.

No comments: