ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 17, 2014

MPYA KABISA: NAFASI ZA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO ZATANGAZWA RASMI LEO HII--16800 WAKOSA SHULE


        

 Nafasi za kujiunga na kidato cha nne mwaka 2014  kwa wanafunzi waliomaliza mwaka jana zimetangazwa rasmi muda huu jijini dare s salaam na naibu waziri wa TAMISEMI  Bw KHASIM MAJALIWA  ambapo zaidi ya wanafunzi 16800 wamekosa nafasi hizo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa shule za kidato cha tano
       Akitangaza majina na shule walizopangiwa wanafunzi hao Mh MAJALIWA amesema kuwa jumla ya wanafunzi 54085 sawa na alimilia 75.61 ya wanafunzi 71527 waliostahili kuingia kidato cha tano mwaka huu wamechaguliwa huku wavulanai ni 31352 wakati wasichana ni 22733 ambapo ni sawa na ongezeko la wanafunzi 20402 kwa kulinganisha na wanafunzi 33683 walochaguliwa mwaka jana.


  Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule mbalimbali wataanza kuripot katika meneo yao tarehe 10 julai mwaka huu ambapo mwisho wa kufika katika shule walizopangiwa ni tarehe 30 julai mwaka huu ambapoamesema kuwa kwa wale ambao watakuwa hawajiripot hadi tarehe hiyo nafasi zao zitajazwa na waliokosa nafasi.


MAJINA NA SHULE ZILIZOPANGIWA WANAFUNZI KWENDA  YATAKUJIA MDA SI MREFU HAPA
 

2 comments:

Anonymous said...

Duh nilipofungua tu moyo ulidunda nikitaka kuona jina la mwanangu sasa umenichelewesha usiku hautakucha hakika. Lini haya maJINA YATATOKA?

Anonymous said...

Kabla ya kutangaza waliochaguliwa , hakikisha kuwa in ten minutes unaweka majina mtandaoni. Education department ya tanzania nayo, kwa namna fulani haiko efficient! tembea nchi nyingine mkajifunze jamani!