Mchungaji Malekela akifungua mkutano wa mgombea wa urais DMV kwa maombi siku ya Jumamosi June 28, 2014 Meadowbrook Park, Chevy Chase, Maryland. Kamati ya uchaguzi imesgeza uchaguzi mpaka Aug 9, 2014 awali uchaguzi huo ulipangwa kufanyika July 20, 2014.
Mgombea wa Urais Liberatus Mwang'ombe akijinadi na kumwaga sera zake.
Wagombea wa makamu wa urais Hariett Shangarai (kushoto) na Salma Moshi katika picha ya pamoja walipokuwa wamehudhuria mkutano wa kampeni wa mgombea urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV Bwn. Liberatus Mwang'ombe uliofanyika siku ya Jumamosi June 28, 2014 katika viwanja vya Meadowbrook Park.
Mgombea wa makamu wa urais Bi Hariett Shangarai akijinadi na kuwaga sera zake kwa wanaDMV.
Mgombea makamu wa Urais Bi. Salma Moshi akijinadi na kuuza sera zake kwa wanaDMV.
Dotto Mallongo akisaidia kumnadi Liberatus Mwang'ombe kwa wanaDMV.
Muna akitoa yake ya moyoni kwenye mkutano wa kampeni ya Uchaguzi wa mgombea wa urais wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
Baadhi ya WanaDMV waliohudhuria mkutano huo.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi.
Picha kwa hisani ya Swahili Villa Blog.
17 comments:
Whoever who was doing this video work is terrible
Darasa la kiswahili HALIJAFA- Walimu wapo na wanafunzi wapo na malengo yapo.Madarasa yamesimamishwa ili kuruhusu utafutaji wa madarasa ya kudumu, na madarasa hayo yakipatikana walimu watatoa tangazo maalum kuhusu utaratibu wa kuandikisha watoto na structure ya shule hii na kuamua kama itaendelea kufanya kazi chini ya jumuiya au kuwa taasisi ya kujitegemea.
Kama una swali lolote kuhusu status ya shule hii tungeomba uwasiliane na walimu wakujitolea hapa DMV.
Hahaha. Sisi tuna washangaa ninyi watu 19 mlionde kumsikiliza huyo kijana.
Kwanza kiongozi hapangi kuvunja katiba. Wewe hujachaguliwa ushapanga kuvunja katiba kwamba hakuna ada. Katiba ndio inavyosema na wala sio hao viongozi waliolianzisha hilo. Hawa ni viongozi wazuri wanaofuata katiba.
Pili wewe kama nonprofit hauruhusiwi kutoa mikopo wala kufanya biashara. Umekaa hapo unazungumza vitu vya ajabu na hao wanakusikiliza. Aibu hamkeni ninyi. Mko Marekani jamani. Yaani uombe misaada ili uwape wana DMV mikopo?.
Tatu. Kama wewe Unataka kuliendeleza Hilo Darasa la kiswahili ambalo umeupongeza uongozi kwa kulianzisha. Sasa mbona umewaponda waanzilishi kwamba kakuna SMART. Nakuhakikishia hata hao walimu ambao wanafundisha hawatokuwa tayari kufanya kazi na wewe kama utashinda. Mdomo wako hauna break.
Sisi tuko marekani. Baada ya kuzungumzia utafanya nini. Unaleta mambo ya kuomba misaada. Kwani tuko Ethiopia hapa. Bora uongozi huu Unafanya Party za mwaka mpya kama source ya income na kuwajumuisha watanzania.
Wewe unaonekana umemorize vitu na wala hujuwi unacho kizungumzia for fact.
DMV mkimucha kiongozi IDDI SANDALY tutalifuatilia chooni.
KUTOKUWA NA MADARASA NDIO KUFA KWA SHULE.MWALIMU UNAWEZA KUTUPATIA WAZAZI TAREHE KAMILI YA SHULE KUFUNGULIWA ? KAMA HAKUNA TAREHE,HAKUNA SHULE.NOW IT IS MORE THAN THREE MONTH HAKUNA SHULE,DARASA.
MTU HUKUWEPO MKUTANONI.WACHA KUPOTOSHA KWA CHUKI ZAKO BINAFSI,MWOGOPE MUNGU KWA KUSEMA UONGO.KWA TAARIFA YAKO WATU ZAIDI YA HAMSINI WALIKUWAPO,WAKE KWA WAUME,WAISLAMU KWA WAKRISTO,WADOGO KWA WAKUBWA.USICHONGANISHE WALIMU NA WAGOMBEA.KAMA WEWE NI MWALIMU NA HUTAKI SERA ZA MGOMBEA USIMPE KURA YAKO PERIOD.
Ukiondoa mchango wa chama how are you going to raise money to fund all those ambitious projects ulizokuwa unabwabwaja hapo Meadobrook Park? Michango ndiyo inatofuatisha wanachama hai according to the katiba, sasa utavunja katiba kwanza sio, halafu ndio utekeleze hizo ambitions zak, right? Do you know how long it will take you to come up with a new Katiba? You better ask somebody. Muda wako wa uenyekiti utamalizika kabla hujapata katiba mpya, unless you want to lead as a dictator. Eti tukupe power of attorney, are you serious? really?
Chuki na udini ndio umewajaa Kama nyinyi atakuwatayali kufundisha wapo Watu wangine watajitolea tu , acheni Chuki binausi na mapezi yasiokuwa na maana yoyote Iddi kafanya nini chamana kweye jumuia hiii
Wewe unaye kuja anonymous hapo juu tunakujua na inaonekana Libe alivyo ongea kuhsu darasa la Kiswahili limekugusa kwani na wewe umeshiriki kulidondosha. Mbona Libe anaeleweka tu kuwa hiyo idea ya darasa ya Kiswahili ni FAILURE kwa sababu kuu moja; DARASA HALIPO TENA NA WALA HALIJULIKANI LITAKUJA LINI. Hii mbona hata mtoto wa darasa la kwanza anaelewa!
Ulivyokuwa mchonganishi na siasa chafu unasema eti Libe anatakam kuvunja katiba, duuuh! kweli watu wengine mpo AMERICA lakini akili bado zipo Tanzania. Mbona libe amesema bila chenga kuwa "ata propose hicho kipengele kivunjwe". Wacha kumuwekea maneno mgombea. Hata aibu huna.
Walimu unao sema hawatakuwa tayari kufanya kazi na Libe na wapi hao. SI wewe tu peke yako ongea kwa niaba yako. Mbona walimu wapo wengi. Kwa nini unakua mgumu kukubali kufeli? Kubali yaishe na jaribu kuboresha.
Inaonekana hujaelewakabisa sera za Libe. Fanya home work dada. Community nyingi zinaendeshwa kwa fundrising na grant proposals. Usivyo na aibu unafurahia party za mwisho wa mwaka kwa sababu unapata tenda na kuwa mtu wa kati. AIBU
Kwa nini usijitokeze kwenye Park kuuliza maswali kama unaona mgombea anamemorize? Umekalia majungu tu unakuja anonymous.
Wacha hizo mama, wewe una wadhifa mkubwa sana kwenye kuwezesha huu uchaguzi
Mnaongelea michango ndio inafanya jumuia ijiendeshe. Kwelli mmeishiwa ideas; muacheni Libe achukue huu jumuia labda atatupeleka mbele. UNATEGEMEA MICHANGO YA WANACHAMA 9 hahahaaaa!
Michango yenyewe hiyo ya wanachama 9 imeishia kwenye vitabu mlivyo weka storage na kuchajiwa $1200.00 . N ahii ndio mnavyo haribu fedha za wanajumuia. Libe kaongea yote; PLAN BILA GOAL NI SAWA NA ZERO.
Darasa la kiswahili lime fell, period. Hamuwezi kudefend hili. Mmewaacha watoto zaidi ya miezi sita sasa, hata mliyo wafundisha wamesajau kwa sasa
Yaani hilo dara likianzishwa tena mnaanza na sifuri. Libe ana point; HAMKUA NA GOOL
SWAHILI PROGRAM IMESHINDWA KWASABABU ILIANZISHWA KWA HULKA. HULKA SIKU ZOTE HAIPELEKI JAMBO KWENYE MALENGO. SABABU CHACHE HAPA CHINI ZILICHANGIA:- 1. VENUE[madarasa] - sina uhakika kama mahali pale palikuwa rasmi kuendeshea program. 2.GHARAMA - inaonyesha hakukuwa na running fund yoyote ya kugharimia program. 3.WALIMU WA KUJITOLEA - inaonyesha walimu walikuwa na moyo tu wa kujitolea lakini uongozi wa jumuiya haukuwa na mikakati mbadala ya kuwawezesha walimu. 4.VIFAA VYA KUFUNDUSHIA - hulka haina muda wakujiandaa, hivyo hakukuwa na uandaaji wa vifaa vya kudumu. Kwa ujumla tunahitaji kujipanga upya sana. UONGOZI WA JUMUIYA HUU UNAOMALIZA ULITEGEMEA BURE AU DEZO ZAIDI,SO WE NEED CHANGE IF WE BELIEVE IN CHANGE. Libe hajasema atavunja katiba bali atashauriana na bodi kurekebisha baadhi ya vipengelle.
Mnalalamika darasa la kiswahili huko nyumbani mnawaongelesha kiswahili? Maana kama wanafundishwa wakitoka inaishia hapo darasani lazima watasahau. Charity begins at home. Na huko majumbani wazazi tuna jukumu kubwa sana la kuwafundisha watoto wetu, na tusitegemee sana watu wengine kufanya kazi yetu. Nimemaliza.
Bwana Liberata mimi ninafurahishwa sana na mfano mzuri na changamoto unayoitoa kwa Uongozi uliopo.
Swali langu ni kwambo, mbona kwenye sala umeifanya ya kikristo tu, na hali unajua community yetu ina waisilamu pia. Hai uwahitaji katika kukupigia kura.
Ningekushauri ulizingatie hilo, kwani ni swala nyeti.
Nakutakia kila la kheri katika jitihada zako za kutaka kuitumikia jamii yako.
WEWE JAMAA ULIYESEMA WATU WALIKUA ZAIDI YA HAMSINI UNAMWAMBIA MWENZIO AMUOGOPE MUNGU KWA KUONGEA UHONGO NA WEWE PIA UNAONGEA UHONGO MIMI NILIKUWEPO NA NILIHESABU WATU WOTE WALIKUA 34 NA MIMI 35 , HACHA HIZO, LIBE HANA YA KUONGEA ANAFUATISHA YA IDDI, HANA JIPYA, MNAWAFUATA MPAKA TAMCO MNAZANI KUTAKUWA NA KAMPENI KULE, HAKUNA UPUUZU TAMCO, HAMTAMSIKIA TENA IDDI, NYIE WALIPIENI WATU TU, KAMA SIYO RUSHWA NINI? IDDI TUMEMSHAURI ASISEME CHOCHOTE KWANI MNAIBA YAKE MNAKUJA HADI NYARUGUSU KUTAFUTA KUNA NINI HAMPATI KITU TAFUTENI YENU
Kwanza wewe libe ulikuwa wapi? Hata siku moja hatujakuona kuwatembelea watoto wa darasa la kiswahili wenzako wamenunua vitabu toka bongo wakaleta, HATUDANGANYIKI!!
you are wasting your time BOY!!!!
Waulize wenzako CCM walikuja na style hiyo hiyo CCM yote ilichukua fomu tulipopata habari wote mufilisi. Hatukaki kuongozwa na network ya chama chochote kile! Tunataka watu neutral kama Hariett na Iddy. Kwa nini msibaki kwenye vyama vyenu vya siasa?
Post a Comment