ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 19, 2014

MTITU ASEMA YAKE YA MOYONI KUHUSU FLORA MBASHA NA MUME WAKE.


HAYA NDO MANENO ALIYO ANDIKA WILLIAM MTITU KUPITIA INSTAGRAM YAKE KUHUSU FLORA MBASHA NA MUMEWE EMMANUEL MBASHA, ANEKABILIWA NA KESI YA KUBAKA.
Ukiiangalia vizuli hii picha utagundua kitu katika macho ya frola mbasha kuna kitu nakiona kinejificha lakini sasa hivi kimeshajitokeza tayali.....hicho kitu ndicho kilichompeleka jera mbasha na asipokuwa makini anaweza asiwe uraiani tena kama ulivyowatokea familia ya nguza .namaanisha mzee nguza na papii kocha wako wapi? Kiukweli frola una roho mbaya ya mwisho kabisa ilichanganyika na ukatili wa mwisho kabisa kiasi kwamba nashindwa kuelewa umeokoka nn ww ? Eti umemrudia YESU ?YESU yupi huyu nnaemwabudu mm au una YESU wako ww na HUYO GWAJIMA wako? Leo umemsahau Mbasha ww ? Wakati alikuokata umechakaa wakati mbasha dereva teksi leo wataka kumfunga ili iwe nn sasa mbasha akifungwa utapata faida gani ww?
Huyo mtoto akija kukuuliza baba yuko wapi utamwambiaje? Fine unaweza kujikaza ukamwambia yuko jera je akikuuliza nani alimshitaki utajibu nn ? Pia waweza kujikaza ukawataja hao wasichana mliowapandikiza je akiuliza ww ulifanya jitihada gani baba asifungwe utasemaje? Hapo auna jibu Acha roho mbaya NENDA KAMTOE MARA MOJA NA MWENDE NYUMBANI MKAONGEE KAMA FAMILIA TWAJUA UWEZO HUO UNAO ILI NA YEYE ATAFUTE HAMSINI ZAKE KAMA WW ULIVYOAMUA KUJISALIMISHA KWA GWAJIMA. USIJE UKASHANGAA WATU WAKASUSIA KAZI ZAKO ZOTE. GDAY.

8 comments:

Anonymous said...

Iachieni mahakama hiyo kesi, kama amebaka au hakubaka itajulikana tu. Hatuwezi kuyachukua na kuyaabudu mawazo ya mtitu kwa kufikiri tu huwezi ukawa na jawabu bila uthibitisho....ukifanya hivyo utaonekana una shida katika akili yako. Mbona Kiswahili unakiharibu wewe mtitu, mahali pa R" unaweka L" pia jina la Flora wewe unaliita Frola" mbona unaharibu majina ya wenzio...je mtu akikuita MTITI badala ya MTITU utafurahia? Kiswahili tu kinawashinda je Kiingereza? TUACHIE MAHAKAMA HIYO KESI YA MTU NA MKEWE NINYI MNAOINGILIA YAWAHUSU NINI? AU MLIKUWEPO?

Anonymous said...

THANK YOU BR. MTITU, HUYO GWAJIMA SI MTUMISHI WA MUNGU SABABU MOJA KUBWA. SIKU FLORA ALIPORIPOTI KWAKE ANGEENDA KWA MBASHA AMA KUMUITA ILI AWAWEKE KIKAO WOTE WAWILI ACCORDING TO BOOK OF MATTHEW 18:15-17, MBASHA ANGEKATAA, GWAJIMA UNGEONGEZA MTUME MWINGINE, HAPO MBASHA ANGEKATAA ANGEFANYWA MTOZA USHURU. LAKINI KANUNI HII MTUMISHI IMEKUSHINDA KWA MANUFAA YAKO BINAFSI, HUO SI UTUMISHI HATA KIDOGO. KUMBUKA KWAMBA FLORA NA MBASHA WOTE NI WAZINZI NA BACKSLIDER, NANI AWASAIDIE? MZEE KULOLA ALIONA MAISHA YA WATOTO HAO MAPEMA INGAWA WAO HAWAKUWA NA TOBA. WACHUNGAJI WASAIDIENI HAO VIJANA WARUDI KUNDINI ILI IBILISI AWAKIMBIE. READ BOOK OF JAMES 4:7-8. ASANTE MUNGU AWAPONYE F NA M KWA UZIMA WA MILELE. AMEN

Anonymous said...

Inasikitisha sana mtu wa dini anamtendea hivi mumewe aliyemsaidia kutoka katika umaskini na kuwa na umarufu alionao hivi sasa.
ndo maana unapochagua mwanamke lazima uwe muangalifu sana na kumuomba mungu akusaidiye upate mke mwema.
mtu wa dini anakuwa hivi je mimi na wewe tusio watu wa dini inakuwaje?

Anonymous said...

Tatizo kaongea ukweli leo hii anaitwa "Roho mbaya" watu kama wewe "MTITU" ndio mnaofanya watu wanaobakwa wasijitokeze kuomba msaada. Hata kama mumewe alimkuta amechakaa sio kumbakia wadogo zake! Badala ya kuanzamkumkashfu Flora acheni sheria ichukue mkondo wake kwanza.

Anonymous said...

Kwa nini mwanaume anapofanya unyama kosa linakuwa la mwanamke? Ama la aliyebakwa au la mkewe. Kwani nyie mbwa haya iwe ukinya kwa jirani mwenye mbwa ndo akazoe? Kama kabaka sheria ichukue mkondo wake, haijalishi kam msichana siyo bikra, haijalishi ni changu, au mtoto, kila mtu ana haki ya kisema NO. Na wanaume tumieni akili zenu acheni kufikiri kwa dhakari zenu, na kusingizia makosa watu wengine, mara alivaa mini, mara kanitega, WTF guys, you have a brain, it is in your head, not your groin!

Anonymous said...

Inanisikitisha sana kuona WaTanzania wasivyo kuwa serious na utawala wa kisheria..kama ni kweli au uongo kwa nini tusiiachie mahakama? Hata Marehemu Michael Jackson alisimamishwa kizimbani kwa kesi ya kuchezea Watoto kijinsia sasa huyu bwana Mbasha yeye ni nani aachwe na Sheria? Halafu tunalia rushwa imetawala bongo wakati hatupendi haki:( kilichotokea ndani ya Nyumba sisi hatukifahamu tusubiri ushahidi na uamuzi wa mahakama ..masikio ya namna hii ni mengi sana kwenye jamii yetuni lazima tuwe makini kwa kutokuyachekea..

Anonymous said...

Kwani ndoa ngapi zina matatizo kama hayo.. tungekuwa wote tunapelekwa waume zetu jela nani angebaki... kwani flora yeye hana dhambi yeyote... mbona haya mambo yanaweza kumalizwa nyumbani tu.. mlokole gani ambaye hawezi kusamehe mwenzake.. kama amemshindwa mume wake si amuache, kwa nini amtese mwenzake.. anaonyesha mfano gani kwa jamii.. Mwenyezi Mungu turehemu.

Anonymous said...

Tusichanganye mada. Mbasha kashitakiwa na Jamuhuri na siyo Flora. Tujiulize hivi mwanao kipenzi akibakwa na mume wa dada yake utayasema unayomwambia leo Flora?
Kwa mtizamo wako mwanamke akiwa kwenye hali duni ukaamua kumpenda anatakiwa alipe fadhila milele. Hata pale unapomkosea na kumdhalilisha anywe maji alale.
Wewe umemuangalia na kumfikiria Mbasha, je umefanya hivyo kwa binti aliyepata matatizo?, jinsi alivyopata majeraha ya kimwili na kisaikolojia.
Wazazi wetu wamepitia mapito sana wengine mpaka wamekufa na wengine wamepata vilema vya maisha. Sababu kubwa ilikuwa ni tabia ya kuwa usiende polisi tuyamalize kifamilia. Mzazi anarudi anaenda kuteseka zaidi au anauwawa kabisa. Imefika wakati tubadilike.
La msingi ni kuwa mahakama ni moja ya mihimili serikali. Hapa mtu ataweka ushahidi wake ili ijulikane kama alikuwa na makosa au la. Na ana nafasi mpaka mahakama ya rufaa. Ukweli tu utajulikana.
Mbakaji yeyote hastahili kupewa nafasi ya kuwepo kwenye jamii, leo kwa Flora kesho kwa Jane