Kwa ufupi
Ni mpango wa kudhibiti Ukawa wasipewe fedha endapo wataamua kususia tena vikao vya Bunge la Katiba
Iringa. Naibu Waziri wa Fedha
na naibu katibu mkuu wa CCM-Bara, Mwigulu Nchemba amesema wajumbe wa
Bunge la Katiba linalotarajia kuanza baadaye Agosti hawatalipwa kwa
mkupuo posho zote za siku 60 ikiwa ni mkakati wa kudhibiti utoro.
Akitoa mkakati huo wa Serikali kwenye mkutano wa CCM uliofanyika Uwanja wa Mwembetogwa na
baadaye Mafinga wilayani Mufindi, Nchemba alisema kikundi cha Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) hawawezi kususia kuhudhuria vikao vya Bunge la Katiba na kulipwa posho kama wajumbe wengine.
“Tukianza tena Bunge la Katiba, nitahakikisha ninabana matumizi na kuamuru fedha za vikao zilipwe kwa awamu na si kwa mkupuo kama wajumbe wanavyotaka hasa wale wa upinzani,” alisema Nchemba ambaye anasimamia sera kwenye wizara hiyo.
Hatua ya Nchemba inatokana na kitendo cha wajumbe 190 wanaounda kutoka vyama vya upinzani na makundi maalum kuamua kutoka ndani ya Bunge la Katiba kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa chombo hicho cha kuandika katiba mpya.
Mwenyekiti wa Ukawa, Freeman Mbowe alisema kuwa wameamua kutoka ukumbini kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo kuwa linajadili masuala ambayo hayakuwasilishwa na Tume ya Jaji Joseph Warioba.
Mbowe alisema kuwa Ukawa wanapinga hoja kujadiliwa nje ya maudhui ya Rasimu ya Katiba hiyo ikiwemo CCM kutaka kuingiza suala la Serikali mbili wakati Tume ya Warioba ilitoa mapendekezo ya Serikali tatu.
Nchemba alisema kama bunge hilo likiendelea na mjadala usio na tija na mizaha, atamshauri Rais Jakaya Kikwete kulifuta kwa kuwa litakuwa linatumia rasilimali za Watanzania bila mafanikio yoyote.
Nchemba alisema alitarajia mijadala ya bunge hilo ingejikita zaidi kwenye mambo ya msingi yanayowagusa wananchi wa kada zote ikiwemo jinsi ya kudhibiti ufisadi kwa kuwa na sheria kali dhidi ya watu hao ili kunusuru uchumi.
Alisema kipaumbele cha Watanzania si muundo wa serikali bali ni maendeleo yao na kuwa Serikali tatu ni gharama kubwa, fedha ambazo zingetumika kuendesha serikali hiyo zingeelekezwa kwenye sekta za maji, afya, elimu na kuwalipa walimu.
Mwananchi.

2 comments:
kwani hizi pesa ni za ccm?
msionjua siasa za bongo ndo mtaka na kumsikiiza huyu kilazi na mpotoshaji ndo maana tanzania inaangamia kwa kuwa na ccm mafisadi na vilazi
Mwigilu, usiwachengua waTanzania. Hivi una uwezo wa aina gani kuwabana wapinzania kifedha? kwani wao sio wanasiasa na wenye vyama? kama CCM ilivyo? Hebu ongeleeni maendeleo ya wananchi na sio siasa za chuki jamani kuna siku CCM itadondoka kifo cha mende sijui utapita wapi!! same thing to Nape!! that is not fair!!!!!!!!
Post a Comment