ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 13, 2014

NANDO ALIBINAFUSISHA PENZI LAKE KWA LULU MICHAEL

Stori: Shakoor Jongo
MTOTO mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ameibuka na kufunguka kuwa amekerwa na kitendo cha mshiriki wa Shindano la Big Brother Africa (BBA) 2013, Amir Khan Nando kujinadi kuwa aliwahi kuwa ‘mtu’ wake kitu ambacho si cha kweli.

Mtoto mzuri Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na Ijumaa kwa juzikati, Lulu alikiri kuwa Nando aliwahi kumtokea na alimkubalia awe ‘my baby’ wake lakini baada ya kumshtukia kuwa hana nia nzuri, alimpotezea kabla hawajazama kwenye dimbwi la mahaba.

“Nahisi Nando alikuwa kwanza anataka kiki kupitia mimi na ndiyo maana kila alipotaka kupiga picha na mimi, nilimkatalia coz nilishamgundua nia yake, nimemshangaa kweli alipotangaza kuwa niliwahi kuwa mpenzi wake labda alivyonitokea na kumkubalia lakini sikufanya naye chochote kinachohusu mapenzi ndiyo akaona aseme hivyo,” alisema Lulu.
Amir Khan Nando akiwa kwenye mahojiano na Global TV Online ndani ya ofisi za Global Publishers

Juzikati, Nando alifanya mahojiano na Global TV Online ambapo awali alidai ‘kutembea’ na Lulu lakini alipobanwa zaidi aliumauma maneno na kudai anampenda na yuko tayari kumuoa kwa sababu ana sifa za kuwa mke (wife material).
Amir Khan Nando akiwa kwenye pozi ndani ya ofisi za Global Publishers:
Credit:GPL

5 comments:

Anonymous said...

Kama brother angekuwa na dolari wala hii issue isingefika hapa...

Anonymous said...

huyu kijana shule zimemshida huko marekani anakuja kujaribu maisha ya maigizo bongo,utaumbuka vijana wa kibongo watakutoa nishai ona hata Lulu mtoto wa darasa la Saba anakutoa nishai na umarekani uswazi wako utaaibika mji huu rudi kwa mama yako

Anonymous said...

nilidhani ni mdosi nilivyoona lile jina siku hizi wabongo bwana hawawezekani kwa kujipa kila aina ya majina na ukabila

Anonymous said...

Baba yake Nando ni Muhindi na mama yake ni mchagga.

Anonymous said...

Jamani Nando hajakulia uswazi. amekua vizuri tu na baba yake na pia mama yake. wa Mikocheni kwa maeneo ya kwa Nyerere tangu anazaliwa pia.