ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 27, 2014

OFISA WA KAMPUNI YA TIGO AKUTWA AKIWA AMEKUFA CHUMBANI KWAKE MKOANI ARUSHA


MFANYAKAZI wa Kampuni ya simu ya Tigo, (MIC T Ltd.),  jijini hapa, Mwita Makore, amekutwa amekufa nyumbani kwake maeneo ya Kimandolu huku akiwa na kamba za viatu shingoni kuashiria kwamba alijinyonga nazo kwa kujitundika kwenye bomba la bafuni kwake.
Hali hiyo imezua gumzo miongoni mwa wakazi wa jiji hili wakihoji inawezekanaje mtu kujinyonga kwa kamba ya viatu hadi kufa huku wengine wakihoji uwezekano wa mwili wa mtu mzima kuning’inia kwenye bomba la bafuni.
Habari kutoka eneo la tukio zinadai kuwa mwili wa Makore ambaye alikuwa kitengo cha ‘store’, ulibainika Juni 20, mwaka huu baada ya kutoonekana wala kupatikana kwa simu zake za kiganjani kwa siku mbili mfululizo, hali iliyowalazimu wafanyakazi wenzake kwenda kumtafuta nyumbani kwake na kubaini kifo chake.
Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo jijini hapa aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina lake, alisema mara ya mwisho Makore kuingia ofisini ilikuwa ni Juni 18, mwaka huu.
“Unajua yeye kazi yake haimlazimu kuwa ofisini muda wote, hivyo akishamalizana na wateja wake huondoka, hivyo siku ya Alhamisi hakuja kabisa ofisini, lakini hakuna aliyekuwa na wazo kama kakutwa na jambo baya.
“Alikuja mteja anayehitaji vocha, ikabidi apigiwe simu, simu ikawa inaita haipokelewi, siku inayofuata wakaja wateja wengine, Mwita akapigiwa simu zake zikawa zinaita tu lakini hazipokelewi.
“Yule mteja akachukia akaamua kupiga simu makao makuu kueleza usumbufu anaoupata, ndipo nao wakawapigia viongozi hapa wakawaeleza kama hapokei simu kwanini wasimfuatilie nyumbani kwake pengine amepata matatizo,” alisema mfanyakazi huyo.
Alisema kuwa walipofika nyumbani kwake walikuta gari ya Kampuni ya Tigo ikiwa imeegeshwa vizuri, lakini funguo zake ziko ndani na milango imerejeshewa tu huku kwenye mlango wa kuingia ndani kwa Makore kukiwa na viatu vyake na walipopiga simu zake, wakasikia zikiita kutoka ndani ndipo wakaamua kuingia ndani.
“Tulipoingia pale mezani tulikuta kuna chupa ya soda, na simu zake tatu pamoja na kadi zake za benki, tukaendelea kuangalia maeneo mbalimbali ya nyumba hiyo ndipo tukamkuta Makore bafuni na kamba ya viatu shingoni,” alisema mfanyakazi huyo wa Tigo.
Mwananchi mwingine anayeishi maeneo ya Kimandolu, alisema tukio hilo limewashangaza sana kwani Makore alikuwa kijana mtaratibu asiye na makuu na alikuwa mpenzi wa mchezo wa pool table.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho alichodai ni cha kawaida kwani amekutwa amekufa nyumbani kwake na hakuna mahali palipovunjwa.
“Achana na habari za barabarani, amekutwa amekufa nyumbani kwake, hakuna mahali pamevunjwa, hiyo ni ‘natural death’,” alisema Sabas 
Chanzo:Tanzania daima

4 comments:

Anonymous said...

huyu sabas chanzo ndo nani? hajalishi mtu akikutwa amekufa kwake na kusema natural death,

wamemchunguza na kumpima na kuona kama ni natural death.story hii ukisoma vizuri utagundua si natural death, mtu alikuwa na tabia njema mstaarabu professional kwa nini awe ananinginia bafuni kwake na kamba za viatu?

kamba za viatu hazi uwi ila kama mtu kamnyonga naye na kumninginiza hapo bafuni.

na katika gari kuna ufungua jiulize ni wangapi wanaacha ufungua ndani ya gari lao na mlango wa gari kusindikiza tu na kuingia ndani mwao kwa hiyari yao,labda kama amelewa sana au kama kuna watu wamo humo wamemteka.

huyu jama sabas chanzo yani hata hawezi kusoma alama za matukio au anaogopa na yeye atakuja kufanyiziwa?

Anonymous said...

Ndiyo maana tukisema jeshi letu halina weledi tunaomba watu mtuelewe. Kwanza mtu amekufa au amejiua haiwezi kuwa "Natural Death" kama anavyosema kamanda huyo wa polisi....hiyo inakuwa homicide au suicide' alichofanya mfanyakazi wa TIGO hakiwezi kuwa Natural death'. Pili huwezi ukatoa conclusion kabla hujafanya uchunguzi wa kitaalamu (forensic investigation) Huu uchunguzi unafanyika ili kuondoa wasiwasi (udhanifu) au doubtness'. Nataka nimweleze huyo kamanda kuwa unaweza ukakuta kamba au bastola pembeni ya mtu aliyejiua lakini uwezekano wa mtu huyo kujiua ni 50% na 50% ni kuuawa. Hivyo ni muhimu kufanya uchunguzi muda wote kabla ya kutoa suluhisho. Inaonekana huko Tanzania wengi walioko magerezani wamefungwa kwa uonevu kama polisi wanafanya uchunguzi wa kubuni.

Anonymous said...

Tumetoa taarifa za mwanzoni "natural death" kutokana na mazingira ya marehemu kukosa michubuko wala dalili za sumu wala uwepo wa chochotr suspecious.
Najua mmejifunza kwa TV wa nje wanavyofanya mambo yao bali hata wao hutoa taarifa za mwanzoni kama hakuna anything suspicious na chochote kikipatikana kuonesha suicide ama homecide jeshi tunao uhuru wa kutoa taarifa nyingine ikiwamo kuwakamata wahusika na kuwapeleka mahakani.
Dont challenge us kwa mnachoona kwa tv kwakuwa hutaweza kuona vyote ama kujua vyote. Go to school TV hazikufundishi kila kitu.
After this preliminary crime site investigation we have our best conclusion until we find anything creepy or suspicious
Tujulishe kama unahusika ama unajua lolote

Anonymous said...

unauhakika gani kama mchangiaji kaona kwa TV?nyie kina nani mpaka tusiwachallenge?na unajuaje kama machangiaji sio msomi?usiropoke tu!watu wanaelimu zao wanawachora tu mnavyodanganya wananchi.tz nitakuja kusalimia na kurudi sina imani na watu waliowekwa kunilinda.