
Nahodha wa zamani wa Nigeria Jay Jay Okocha amemlaumu kocha Stephen Keshi kwa timu yake kushindwa kucheza vizuri katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia kundi F dhidi ya Iran siku ya Jumatatu.
Timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.
"Huu ulikuwa mchezo ambao lazima tushinde. Hatukufanya vya kutosha, tulicheza chini ya kiwango," amesema Okocha.
No comments:
Post a Comment