Mwili
wa Marehemu George Tyson Ukiwasili Viwanja vya Leaders Jijini Dsm
kwaajili ya Kuagwa na hatimaye Kesho Kusafirishwa Kuelekea Nchini Kenya
kwa Mazishi(Mazishi huko Kenya yatafanyika Tar 14/06/2014.
Mwili Ukipelekwa eneo Rasmi la
Kuagia Wananchi.Mwili Umeshawekwa eneo lililoandaliwa kwaajili ya Kuaga.
Msanii Monalisi Mke wa Kwanza wa Marehemu akiwa na Mtoto wake aliyezaa na Marehemu George Tyson.
Mkuu wa Mkoa wa DSM.
Mboni akiwa kwenye Majonzi Makali sana ya Kupotelewa na Director wake Marehemu George Tyson.
Simanzi na Vilio Vimetawala kwa hawa watu wa Karibu kabisa na Marehemu George TysonMke wa Marehemu George Tyson akipozwa na Ndugu wa Marehemu.
Mwenyekiti wa Bongo Movie Steve Nyerere akiteta Jambo na Mkuu wa Mkoa wa Dms.
Sehemu ya Waombolezaji.
Uimbaji Ukiendelea Kusifu na Kumtukuza Mungu.Eden THE Rocker akiwa na Familia ya TV 1 wakati wa Kuuaga Mwili wa Marehemu George.
Wanafamilia wa TV1 alikokuwa anafanya kazi Marehemu.Msanii Zola D KIng ambaye anafanya kazi TV1 kwenye Kipindi cha Boys Boys akijumuika kwenyee Msiba huu.
Bongo Movie Family
Mkuu wa Mkoa akuwasihi Wasanii nchini kuendeleza Umoja wao katika shida na Raha kama wanavyofanya sasa.Waombolezaji.
Muwakilishi Kutoka Mwanza upande wa Filamu akitoa Rambirambi.Dj Choka akiweka Sawa Mashine yake kwaajili ya Kunasa Matukio.
Huyu
anaitwa MWAIPOPO aliwakilisha Kutoa neno kwa Niaba ya Marafiki wote wa
George Tyson,Hakika alishindwa Kuzungumza Kutokana na Uchungu alioupata
kwa Kumpoteza Mtu Muhimu na wakaribu kama George.
Kuna wakati Mboni alilia sana Na Kuhitaji Kupata Maji.
Mtangazaji
Joyce Kiria akitoa Neno kwaajili ya Marehemu,Ikumbukwe Marehemu George
Tyson Mzaliwa wa Kenya ndiye alianza Kuongoza Kipindi cha WANAWAKE LIVE
siku za awali.
Mkuu wa Mkoa akibadilishana Mawazo na Uncle Lundenga HashimBoss wa Michuzi Media Uncle Michuzi akibadilishana Mawazo na Asha Baraka
Mkali wa Social Network Le Mutuz akiwa na Wakali wa Bongo Movie.Msanii Roma Mkatoriki pia ameshiriki Zoezi la Kuuga Mwili wa Mpendwa wetu George Tyson.Zola D King.Msanii TEA(Kulia) akibadilishana na Mawazo na MwenzakeMkubwa Ruge Mtahaba akibadilishana Mawazo na Hashim Lundenga.Mchungaji
akiombea Safari ya Marehemu George Tyson,Pia ameombea Wasanii Kuamini
kwa Mungu na sio Miungu katika Kipindi hiki Kigumu.Maombezi yakiendelea na Kuvunja Nguvu za Giza na Pepo la Vifo ndani ya Bongo Movie.Waombolezaji waktoa Sadaka Maalum kwaajili ya Kuchangia Malezi ya Watoto wa Marehemu.Steve
Nyerere,Mwenyekiti wa Bongo Movie akizungumza na Wasanii pamoja na
Waombolezaji wengine,Kubwa amesisitiza Kuamini Mungu tu,Kuamini Miungu
ni Kupoteza Muda na hakusaidii Chochote Kile.
Hawa ni Baadhi ya Wasanii waliozaliwa Kisanaa Mikononi mwa Marehemu George Tyson.
Msanii Elizabeth Michel akichat Kidogo wakati Shughuli ya Kuaga Mwili wa Marehemu Ikiendelea.
Mtoto wa Marehemu George Tyson aliyezaa na Monalisa akisoma Ujumbe kwaajili ya Baba Yake.Inauma Kumpoteza Mzazi.Chini ni Mke wa Marehemu aliyekuwa anaishi naye hadi Mauti Yanamkuta.
Meya Jerry Slaa akizungumza na Waomborezaji.
Mwili wa Marehemu George Otieno Okumu .Mboni akiaga Mwili wa Mpendwa wake George TysonMkubwa Ruge Mtahaba.Mtangazaji Maimatha Wa Jesse
Mtangazaji Jerry Muro akitoa Heshima za Mwisho.
Mke wa Marehemu akibusu Mwili wa Mme wake aliyekwisha Lala Usingizi wa Milele Marehemu George Tyson.
Joyce Kiria akimuaga George.
Mtoto wa Marehemu akimuaga Baba yake.
Monalisa aliyekuwa Mke wa Marehemu George akiaga Mwili wa Marehemu.
Kuna Watanzania wengine walishiwa Nguvu na Kuzimia kwasababu ya Majonzi ya Kumpoteza Marehemu George Tyson.
Mwili
Ukiondolewa Viwanja vya Leaders kwaajili ya Kupelekwa Uwanja wa Ndege
na Kesho saa 4 Asubuhi utasafirishwa kwenda Nchini Kenya Nyumbani kwa
akina George kwa Mazishi yanayotegemewa Kufanyika Tar.14/06/2014 na
Tanzania Wawakilishi Watatu,MMoja ni Rais wa Bongo Movie Tanzania na
Wajumbe wawili Kutoka Mboni Show.
Tafadhali Ukiamua Kuchukua Picha hizi na Kuzitumia andika Ulikozitoa(Soma Chini hapa).
Picha/Maelezo na Festo Sanga wa Habari Kwanza Media/Vijimambo Blog.
REST IN PEACE GEORGE OTIENO OKOMU
3 comments:
Sasa mm nashindwa kuelewa hivi ni watu wangapi maarufu waliotutoka hapa duniani mpaka leo hii ionekane kama miujiza? Hao wanaojifanya kupoteza fahamu ni wauza sura tu mbele ya hivyo viblog vyenu,,na hivi mnajua kama wakenya hawakupendeni hata kidogo? Na je huyu angekua mtz kule kenya watu kule wangejaa hivyo? Jibu hapana,,mm napita njia tu huku nikiamini mungu yupo na kifo kipo,,kinachotakiwa tutubu kwa mungu wetu coz ....zimezidi.na hii tabia ya kwenda msibani huku ukiwa umejipura wala haiendani kabisaaa msibani ni sehemu ya huzuniiiiiii
MH!
Nawapeni pole nyingi sana wafiwa wote jamani mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Safari bado ni ndefu ya kuelekea Kisumu nchini Kenya kumpumzisha mpendwa wetu kwenye nyumba yake ya milele, hivyo watoto wake na watoto wake nawaombea mungu awape nguvu na uvumilivu katika hali zote.
Naomba sote tuamini kwamba ratiba za mungu haziingiliwi wala hazibadilishwi, hivyo kwa mungu ilishapangwa kwamba siku, tarehe na mwaka fulani ndugu yetu ataanza maisha mengine ya uko kwa muumba.
Tunawaombeeni familia muwe na upendo, mshikamano na maelewano na hasa katika kuwalea watoto wa marehemu. Washikamanishe watoto na hasa ikizingatiwa kuwa ndugu zao upande wa baba yao wako mbali nao (Kenya), sasa kazi kwenu nyie mama zao kuelewana na kuwa mnawapeleka watoto walau mara moja moja kwao. Ni ushauri tu si lazima iwe hivyo.
Pole kwa mara nyingine tena wapendwa familia ya marehemu.
Post a Comment