SERIKALI
imesema Tanzania haina haki miliki ya jina la mlima Kilimanjaro, hivyo
mashirika mbalimbali yanaweza kutumia nembo ya jina hilo katika
kutangaza vivutio vya utalii kama Shirika la Ndege la Kenya, Kenya
Airways linavyodaiwa kutumia nembo ya Mlima huo.
Mwanasheria
Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema, ameliambia Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania leo Jumanne Juni 17, 2014 kuwa kitendo cha Shirika
hilo kutumia nembo ya mlima huo hakina madhara yoyote kutokana na kuwa
hakuna aliye na hati miliki ya jina la mlima huo.
Amesema,
jambo hilo linatakiwa kutofautishwa na haki miliki zinazotumika kwenye
vitabu mbalimbali vinavyoandikwa na waandishi katika jamii na zile
zinazotajwa kwenye kazi za sanaa kutokana na lengo la kutumia nembo
hiyo.
KQ-Kilimanjaro-texts
“Ni kweli kuwa kuna Ndege ya Shirika la Kenya inayotumia maandishi ya
'Mlima Kilimanjaro' lakini sio kosa kwasababu hakuna mtu aliyepatient
kwa ajili ya mlima huo katika Ndege; kama sisi tungekuwa tumefanya kabla
yao ingekuwa sawa, lakini pia ili ufanye hivyo ni lazima utumie ujuzi
wa Interestial property na hii haihusiki ni haki miliki, ambayo
inatumika kwenye vitabu na kwenye mambo sanaa” Kauli ya Serikali
inafuatia swali lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne
Kilango, ambaye alisema “Mataifa mengi yanatumia Ndege zao kutangaza
vivutio vya utalii wa ndani kama vile Air Tanzania inavyotumia nembo ya
Twiga na nadhalika ili kutangaza utalii huo, lakini kwanini Ndege ya
shirika hilo inautangaza mlima Kilimanjaro kama ni wa kwao? Je, suala
hili serikali inatoa kauli gani kwa kuwa suala hili sio sahihi”
alikaririwa.
kumekuwepo
na mjadala mzito wa chini chini katika kipindi cha muda mrefu kuwa nchi
jirani ya Kenya imekuwa ikijinadi katika mataifa mbalimbali kuwa
inamiliki mlima huo na baadhi ya rasilimali zilizopo kando kando ya
mlima huo na maeneo mengine, suala ambalo limetafsiriwa kuwa Kenya
inajinufaisha kupitia rasilimali za Tanzania visivyo halali.

2 comments:
Kama tatizo ni patent basi tuandikishe na maneno yaishe...lakini kulalamika kwa nini KQ wanatumia hiyo nembo siyo sababu ya kimsingi infact tunaweza kuonekana tuna wivu au chuki binafsi na Kenya Airways. Nasema hivyo kwa sababu KLM wana ndege mbili, moja inaitwa "Mount Kilimanjaro" na nyingine inaitwa "Serengeti" na zote hizi zimewahi kuja hata Tanzania, ila hakuna aliyelalamika, tena wakati Serengeti imetua Kilimanjaro kulifanyika hafla ya kuipokea hiyo ndege maana ilikuwa ndo kwanza imetoka kiwandani....Je hatukugundua hayo tangu mwaka 2005 ndo tuanze kuilalamikia KQ leo? Au tuna sababu/chuki nyingine na KQ....kama hatupendezwi na marketing skills zao then may be we need to step up our game
Mdau

Post a Comment