Kikosi cha Uingereza
kitakachopambana kwenye kombe la dunia kimewasili nchini Brazil mara
baada ya kupaa na ndege mpaka Amerika ya kusini kutoka Florida kufuatia
sare ya bila kufungana dhidi ya Honduras.
Kocha,Gary Neville aliongozwa chini ya chama husika katika kupiga
hatua kwenye uwanja wa ndege wa Rio de Janeiro pamoja na beki,Gary
Cahill ambaye ndiye mchezaji wa kwanza kuondoka na ndege mara baada ya
kupaa kwa masaa nane na nusu kutokea Fort Lauderdale.
Kikosi hicho kwasasa kitaweka makazi katika mji wa Rio mara baada ya
kusafiri kwa gari kwa mwendo wa saa zima kutokea uwanja wa ndege.
Meneja,Roy Hodgson atakiongoza kikosi chake katika kufanya mazoezi ya
Jumatatu asubuhi yakifuatiwa na mapumziko ya siku ya Jumanne asubuhi.
Kikosi kitafanya tena mazoezi siku ya Jumatano asubuhi kabla ya
kupanda ndege mpaka Manaus siku ya Alhamisi kwaajili ya kujiandaa na
mchezo wao wa kwanza wa kundi D dhidi ya Italia utakaopigwa Jumamosi.
Kutakuwa na sehemu ya mazoezi ndani ya Manaus siku ya Alhamisi Jioni
na mkutano wa waandishi wa habari siku ya Ijumaa ikifuatiwa na sehemu
nyingine ya mazoezi ya maandalizi ya mwisho.
Uingereza wataanza kampeni zao za kombe la dunia dhidi ya Italia katika dimba la Arena Amazonia usiku wa Jumamosi ijayo
No comments:
Post a Comment