ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 17, 2014

TIMU YA TANZANIA MOVIE TALENTS YAFURAHIA KUUNGANA TENA NA JAJI MONALISA BAADA YA KUREJEA KAZINI LEO ASUBUHI


Yvonne Cherry au Monalisa akiwa kwenye meza ya Majaji Asubuhi hii mara baada ya kurejea Kazini.

Baada ya Kumalizika Kwa Msiba wa Marehemu George Tyson ambae alikuwa Mzazi Mwenza wa Jaji wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT), Bi Yvonne Cherry au Monalisa amerudi tena kazini leo asubuhi na kuendelea na Majukumu yake kutokana na shindano la Tanzania Movie Talents kusimamishwa Kwa muda kutokana na Msiba huo uliotokea wiki kadhaa zilizopita.

Timu ya Tanzania Movie Talents (TMT) inafurahi sana kuungana na Jaji Monalisa katika majukumu ya kila siku ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT).

1 comment:

Anonymous said...

Yvonne Cherry, mwanangu, pole sana kwa msiba wa mzazi mwenzako, George Tyson. Mimi mama yako mkubwa, mama zako wadogo, na wajomba zako wote tulioko US, bila kumsahau Bibi yako tunamwomba Mungu aendelee kukupa nguvu wakati huu mgumu wa msiba.