ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 3, 2014

TUKIO LA AJABU LINALOHUSISHWA NA USHIRIKINA KAZINI, LATOKEA LEGHO SINZA!


Mwathirika akisugua miguu chini kama vile anawashwa na vitu mwilini.
 
MTU mmoja ambaye anasadikiwa kula chakula na baadaye kuanza kuchanganyikiwa alinaswa na kamera yetu leo akisugua miguu ardhini na kujikuna mwili mzima, jambo ambalo lilidaiwa na wapita njia kuwa alikuwa amekula chakula kilichokuwa maalumu kwa ajili ya kafara.  
Haikujulikana chakula hicho amekila wapi na ni chakula gani.  Jina lake pia halikuweza kupatikana mpaka kamera yetu inaondoka sehemu hiyo.
Tukio zima limetokea eneo la  Sinza-Legho Mtaa wa Shekilango, jijini Dar es Salaam,  kwenye kampuni ya magari makubwa ya usafirishaji.
(Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)

1 comment:

Anonymous said...

JE mtu huyu hawezi kuwa na allergy ya chakula hicho kwani kuwashwa mwili na kujikuna na pengine hata anavyosugua miguu ni kusaidia kujikuna, mbona tuna haraka sana ya kukubali imani potofu?