Picha ya mwisho ya Hayati Baba wa Taifa
Julius Kambarage Nyerere aliyopiga kijijini kwake Butiama kabla ya
kwenda kupata matibabu nchini Uingereza ambapo alifia katika Hospitali
ya Mt. Thomas.
Mmisionari Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye
anasambaza ujumbe kuhusu hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere
kuwa Mtakatifu wa 21 tangu tarehe 20/03/2013.
Wakati yote haya yakifanyika kutoka nchini Uganda: Rais Yoweri
Museveni, amesema kiongozi bora ni yule anayefuata maagizo ya Mungu na
kuwatumikia binadamu wote kwa usawa na haki.
Rais Museveni aliyasema hayo Tarehe moja mwezi June, wakati wa ibada
ya kuombea mchakato wa kumfanya Marehemu Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere kuwa mwenyeheri na hatimaye kutangazwa mtakatifu.
Picha
ya mchoro wa Mtakatifu Charles Lwanga aliyemtangaza Hayati Baba wa
Taifa kuwa Mtakatifu wa 21 ambapo alisema hata kwenye maandiko
matakatifu ya Biblia kuna mistari inayomtaka binadamu ampende binadamu
mwenzake kama anavyojipenda yeye.
Rais Museveni alisema anatarajia kupeleka
ushahidi kwa Papa Benedict kwamba Mwalimu Nyerere ana sifa za kutangazwa
kuwa mtakatifu kwa sababu alimtii Mungu na kuwatumikia binadamu.
Mmisionari
Simon Nyirani Mhagama wa Shirika la Mt. Kalorilwanga ambaye anasambaza
ujumbe kuhusu Hayati Baba wa Taifa Julius Kambarage Nyerere kuwa
Mtakatifu wa 21 akiwa katika picha ya pamoja na watoto waliotembelea
kaburi la Baba wa Taifa Butiama mkoani Mara.
Kufuatia hatua hiyo ya kwenda Roma kutoa ushahidi, Rais Museveni
amesema katika maadhimisho ya kuombea mchakato wa Mwalimu kuwa Mtakatifu
yatakayofanyika mwakani, ameahidi kuwaita maraisi wote waliowahi
kufanya kazi na Mwalimu Nyerere ili kuuthibitishia ulimwengu kuwa
Marehemu Baba wa Taifa ameweza kuwa unganisha Waafrika.
Alifafanua kuwa Mwalimu ametoa mchango mkubwa wa ukombozi kwa nchi za
Msumbiji, Zambia, Zimbabwe, Namibia, Angola, Afrika Kusini, Uganda na
Tanzania yenyewe. Hivyo kuja kwa viongozi hao kushiriki ibada hii
itakuwa Baraka kubwa.
No comments:
Post a Comment