| Akikabidhi seti moja ya jezi, katikati ni mdhamini wa kombe hilo Jackson Kiwaga |
| Hapa alikabidhi zawadi ya seti moja ya jezi kwa mshindi wa pili Nyabula FC, mwenye kofia nyeupe ni mdhamini wa ligo hiyo Jackson Kiswaga |
| zawadi ya pili kwa mshindi wa pili ulikuwa mpira |
| waamuzi wakifurahi baada ya kumaliza mpambano huo salama |
| moja ya tukio katika mchezo huo, hapa golikipa wa Nyabula akiutazama mpira uliozama katika lango lake huku akionesha kukata tamaa |
| Kikosi cha Ugwachanya kikifurahi |
| Golikipa wa Nyabula kala pozi lililoashiria mchezo huo umekwisha |
| sehemu ya mshabiki waliojitokeza |
PAZIA
la
ligi daraja la tatu wilaya ya Iringa Vijijini lililoshirikisha timu 12
limefungwa wakati
wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika juzi kwa timu ya
Ugwachanya FC kuibamiza bila huruma mabao 3-0 klabu ya Nyabula FC.
Mchezo
huo uliohudhuriwa na mamia ya wakazi wa kata ya Tanangozi na vitongoji vyake
uliokuwa na shamrashamra za aina yake kutoka kwa mashabiki wa timu zote mbili.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Simu za Mkoani ya TIGO Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Jackson
Kiswaga ambaye pia ni mdhamini wa ligi hiyo ameahidi kuongeza dau la udhamini msimu
ujao wa ligi hiyo ili kuiongezea hadhi.
Kwa
ushindi huo, Ugwachanya FC ilipata kikombe na seti moja ya jezi huku Nyabula FC
ikijipatia seti moja ya jezi na mpira.
Dalili
za Ugwachanya FC kuwa bingwa wa ligi hiyo ilidhihiri katika dakika zote 90 za fainali
hiyo baada ya wachezaji wake kuutawala vyema mchezo huo.
Goli
la kwanza la timu hiyo liliwekwa kimiani katika dakika ya 14 baada ya
mshambualiji wake Oscar Mhelela aliyepokea pasi ndefu kutoka Baraka Cheyo
kuwahadaa walinzi wa Nyabula FC na kupiga shuti kali lililomshinda golikipa wa timu
hiyo FC Fred Chilala.
Katika dakika 30 ya mchezo Ugwachanya FC iliongeza
bao la pili kupitia kiungo wake mshambuliaji Nasibu Ndauka aliyehitimisha karamu
ya mabao ya timu hiyo katika dakika ya 34 kwa kufunga bao la tatu.
Hasira
za timu ya Nyabula kuchabangwa ilitaka kuiharibu fainali hiyo baada ya
kujitokeza baadhi ya mashabiki wa timu hiyo kuvamia meza kuu na kumtuhumu Katibu
wa Chama cha Soka cha Wilaya hiyo, Juma Lalika kuhusika kuihujumu timu yao kwa
kuruhusu wachezaji ambao hakuwasajiliwa na Ugwachanya kuichezea timu hiyo.
Hasira
zilizidi zaidi katika daakika 55 ya mchezo huo baada ya mshambualiji wake
Fadhil Nganga kukosa penati waliyotunikiwa ikiwa ni matokeo ya mchezaji wake
Octavian Balama kuchezewa rafu katika eneo la hatari.
Mratibu
wa kombe la Muungano, Daudi Yasin alikuwa mgeni rasmi wa fainali hiyo na baada
ya kukabidhi zawadi kwa washindi alisema mashindano hayo yatasaidia kukuza
sekta ya mpira wa miguu mkoani Iringa.
Ugwachanya
FC; Good Kibiki, Paulo Malekela, Method
Mkonnda, Oscar Mhelela, Salum Mapunda, Steven Mhelela, Veda Kiwele, Baraka
Cheyo, Nasibu Ndauka, Kingunge Ndenga na Austin Mlwale.
Nyabula
FC; Fredy Chilala, Pascal Luluzile,
Yohel Mashaka, Benson Mlawa, Fadhil Ngaga, Joseph Mlawa, Said Kigomba, Amazon
Lundimba, Exaud Kaduma, Octavian Balama na Gerald Nganga.
No comments:
Post a Comment