Advertisements

Sunday, June 15, 2014

USIKU WA WANAWAKE WA TANZANIA WAFANA, BALOZI AWAFAGILIA TANO LADIES

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwasili kwenye ukumbi wa Martin's Crosswinds uliopo Greenbelt, Maryland kwenye usiku wa Wanawake wa Tanzania ulioratibiwa na kikundi cha wakinamama wa tano chenye maskani yao DMV kinachobeba jina la Tano ladies na kuufanya usiku huo kuwa wa aina yake na kuweka historia ya wanawake nchini Marekani kwa kusahau tofauti zao, kuwaacha wapendwa wao nyumbani na kuwa kitu kimoja kwa kujumuika pamoja kuelimishana juu ya kupendana na kuungana mkono kila mwenzao anapofanya jambo jema.  
Meza alioyokaa Mhe. Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkuu wa Utawala na Fedha, Mama Lily Munanka akijumuika kwenye usiku wa wanawake wa Tanzania uliofanyika siku ya Jumamosi June 14, 2014, Greenbelt, Maryland.

Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiongea machache kwenye usiku huo na kusisitiza upendo, ushirikiano na mshikamano kwa akina mama na kuwashukuru tano ladies kwa kuja na mawazo ya kuunda kikundi chao kwa lengo la kuwaunganisha wanawake wa Marekani na baadae aliwatunukia zawadi toka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.

Haika Lawere ambaye ni mkurugenzi na mmiliki wa Mbezi Garden Hotel Ltd Tanzania mpenda maendeleo ya akina mama akiongea na kuwaelemisha akina mama juu ya kupendana na kutokuwa na choyo ya kunyimana fulsa za maendeleo na kuwasihi wanawake waache raho za kwanini daima tuwe na wivu wa maendeleo sio wivu wa kurudishana nyuma.

Miriam Kinunda mwandishi wa kitabu cha Taste of Tanzania akielezea sababu za yeye kuandika kitabu chake kwa lugha ya kiingereza kwa kusema sababu kubwa ilikuwa ni kujulisha ulimwengu juu ya mapishi ya Tanzania na kwa kuwa nipo nje ya Tanzania na lengo ya kitabu changu ilikuwa kukiuzwa nje ya Tanzania na akatoa mfano wa Mapishi ya China kama yangekua yanaandikwa Kichina hadhani kama Dunia ingekua inajua mapishi ya Fried Rice.
Juu na chini Balozi wa Tanzania nchini Marekani akiwazawadia Tano Ladies
Mwenyekiti wa Tano Ladies Asha Hariz akitoa shukurani kwa wanawake wote na kuwashukuru kuwaunga mkono na kukubali wanachofanya.
Asha Nyang;anyi mmoja wa Tano Ladies akiwashukuru wadhamini.
Tano Ladies katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

16 comments:

bazazi said...

Great job DMV woman's ... Wanawasemi
Hamjuwi kuvaa this was super &classy KEEP THIS WAY ALL THE TIME .. DMV standup

Anonymous said...

Jacky Korassa wewe mzuri sana jamani yaani uzuri wako hakuna DMV I swear.

Anonymous said...

Haika Lawere!! Nimekupendaje sasa! Jamani umeji present jinsi ulivyo!! Na SAUTI yako na unyenyekevu !! No wonder unafanikiwa !! Wengine Pia nzuri !! Ila mama Mushala unge ignore mambo mengine , na mipasho kuachia wengine !!! Mmmhhh! Hata waliokomenti ujinga wamefurahi umewa acknowledge !! Nadhani my Tano Ladies mtasonga mbele tu, kila mnapoona mapungufu yenu na kujirekebisha!! Kumbukeni mnaongea na kina mama wenzenu , ambapo vi mood swings vinahusu!!! Humbleness Muhimu !!

Anonymous said...

Tano ladies oyeee!,,, mnijuze tu urembo wa sura! Lol! 'twas a night to remember! Thank u ladies,mbarikiwe!

Anonymous said...

Asha hariz ndio alipendeza kwenye tano ledies .

Anonymous said...

Asha hiriz mzuri na anashepu na kapendeza.

Anonymous said...

Nice job tano ladies jacky korasa u so beautiful darling mmmwaaah ......mdau Boston.

Anonymous said...

dini na dunia, is a different way, katika mafundisho ya dini waislam wana utamaduni wao wa kuvaa hasa katika kadamnasi ya watu, dada yetu unaitisha mighadhara ya kidini hali ya kuwa wewe mwenyewe uko nusu uchi kwa mafundisho na imani ya kiislam, sura gani unawaonyesha hasa wale unaowaitisha katika masuala ya dini, dada yetu muogope mola wako dunia ni ya kupita, hakuna wa kukusifu ila sifa ni zile alizotatakishwa allah (SWA)motto wa kiungwana unauwelewa wa dini kwa kiasi chako, muogope mola wako

Anonymous said...

Aliyependeza ni Renee baby cakes peke yake, pamoja na baloz tuu!!!! Wengine cjawaelewaa..

Anonymous said...

Naona ulipitwa na mada zilizotolewa usiku huo. Dada Haika ameeleza haya ya sijui fulani kavaa vizuri/vibaya inakuhusuje??? How much do u get for time/energy spent? TUBADILIKE WANAWAKE WAKIBONGO KHAAAA!!!!!!Jitahidi kuwa na " ABUNDANT MIND" & not SCARCE MIND kama alivyosema da Lawere!!!!! NAWAPENDA SANAAA TANO LADIES!!!

Anonymous said...

Ambacho sikukielewa Tano Ladies mnaleta Msenaji kutoka Bongo atatupa ushauri gani huyo? She is CULTURALLY INCOMPETENT!!!! Weka wamama wa hapa USA wapiganaji wa maisha ngangali ya majuu, luna walioanza maisha kwa kupika ubwabwa sasa wana makampuni hao ndio wa kutueleza madude!! Sio hoa wanaoishi nyumba za bongo za urithi na kufanya kazi za kutafutiwa!!!
Shame on you TANO LADIES!!!
Luka usibanie hii kwa kuogopa kusutwaa!!

Anonymous said...

Tano ladie mbona hamuonekani Happy au hamkupata faida,kwa hiyo faida kulipia macredit Kadi,poleni ndio kubwa huo

Anonymous said...

Omby umependeza sana I like u so very much keep it up.

Anonymous said...

Lmaooo huyu renee kapendeza nini , na mimba yake ili aolewe.....nafwaaaa mie, hebu nipishe mie

Anonymous said...

Mwenzetu wa June 15, 11:11PM, Ujumbe wa Haika hauna mipaka ni how you see the God's Blessing.. kwa kufafanua about our Mind sets.. the way we see tunavyojaaliwa na Muumba Wetu.. kuna Abundance Mentality na Scarce Mentality.. That speech was timeless and boundary less.. hata kama unakaa chini ya jiwe.. utaelewa kwamba Mungu ameumba na ametuwekea Neema zake kwenye kila kitu.. cha kufanya ni kufungua Mioyo Yetu na Kuona God's abundance that already are here for us.. tuwache roho za uoga (scarce mentality) Mungu will provide abundantly once you are ready to receive..
Ni muhtasari wa Msemaji wetu na kwa kuwa ametoka nyumbani sio kudharua.. Unanifanya nijiulize kweli ulikuwepo pale kweli?.. mhhh! we haya weee..

Upendo na Umoja!.. Wadumu Tano Ladies..

Anonymous said...

Kama kawaida wapo waliokuwa wanashika mkia darasani maana hata mwalimu afundishe vipi THEY DO NOT GET IT!!!! Message delivered! Yale yale aliyosema mama Mushala kuwa kabla hujakaa na kuwasagia TANO ladies au Haika jiulize je what's wrong with me?? Walioongea ni watu wengi na ni mtu mmoja tuu is from Tanzania na wote waliobaki ni wa hapa Marekani sasa wewe unayeandika maneno mabaya kuhusu HAIKA ungeweza hata kuongea chochote cha maana??? ACHA WIVU WANAWAKE WOTE WALIOONGEA WAMEONGEA UKWELI HAYAKUHUSU KAMA ALIYEONGEA KATOKA CHINA JAPAN AU HEAVEN!!! SWALI NI KUJIULIZA, JE MIMI MUNGU KANIPA NINI ILI NIKITUMIE POSITIVE NIJINYANYUE MWENYEWE NA WENGINE, WE SHOULD ALL SAY ITS SHAME ON YOU TO WRITE SUCH PUMBA!!

"EMPOWER, INSPIRE AND MAKE CHANGE TO YOUR LIFE". TUMIA HIZI BLOGS KUTANGAZA KIPAJI MUNGU ALICHOKUPA..