Kuna fukuto la wahamiaji wasio na vibali takinaka, wanaofurika kwa wingi kutoka kwenye nchi za kati katika bara la Amerika ya Kusini kuingia nchini Marekani.
Sasa maji yakizidi hayana budi kupwa na hivyo majimbo yote ya mpakani
mwa Mexico hasa jimboni Texas yameelemewa kiasi cha maofisa wa uhamiaji
kuamua kusafirisha wahamiaji hao kwa kutumia
basi na ndege na kuwabwaga katika vituo vya mabasi ya Greyhound hapa Arizona.
basi na ndege na kuwabwaga katika vituo vya mabasi ya Greyhound hapa Arizona.
Jambo hilo limembugudhi Gavana wetu hapa Arizona, Jan Brewer ambaye ameamua kumlima barua Rais Barack Obama akitaka maelezo ya ni kwa nini watu hao wawekwe hapa bila yeye kupewa taarifa wala maelezo yoyote.
Watu hao wameachwa katika vituo hivyo bila ya huduma yoyote ile muhimu
si ya chakula wala malazi. Kinachofanyika sasa ni mashirika ya
kibinadamu na watu binafsi kujitolea kila walicho nacho kwa ajili ya
kuwasaidia watu hao ambao wengi wao ni wanawake na watoto.
Kama vile kuwabwaga juzi na Gavana Brewer kutuma barua inayohitaji majibu haikuwa lolote wala chochote, leo tena kundi jingine la wahamiaji limetelekezwa kwa mtindo wa 'tudaidiane' baada ya maofisa wa Texas kusema wameelemewa na wanahitaji usaidizi kwa kuwa hili si jambo geni kufanyika.
Wakazi wa hapa wanaofuatilia sakata hili wanajiuliza, je, kuna nini kinachoendelea katika nchi wanakotoka wahamiaji hawa kinachowasababisha wamiminike kwa kasi?
Baadhi ya wahamiaji waliohojiwa wamesema walilazimika kuja Marekani kwa
sababu familia zao ziliwasukuma kufanya hivyo kwa kuwa wenzao wanaoingia
Marekani wanapata misukosuko ya hapa na pale ila baada ya muda
wanafanikiwa kukaa na kufanya kazi na kuwasaidia waliobaki nyumbani.
Kuhusu ni kwa nini wengi wa wahamiaji hao ni wanawake na watoto,
wanasema waliambiwa hayo ndiyo makundi ya watu ambao 'wanahurumiwa' na
ni rahisi kupewa misaada ya kujikimu ili kujiwezesha kimaisha, hivyo
karibu kila familia yenye mke na watoto walishinikizwa kusafiri kuja
Marekani.
Gavana Brewer akishirikiana na vikosi vyake wamefanikiwa kwa kiwango
kikubwa kuzuia wahamiaji wasio na vibali wakati hali ni kinyume katika
jimbo la Texas.




1 comment:
nchi yenyewe marekani kuwaonea huruma wakina mama kakwambia nani? wanateseka huko kama nini wenyewe wazawa itakuwa wao
Post a Comment