ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 12, 2014

Wambura sasa ruksa kuwania urais Simba

Dar es Salaam. Kama ilivyotarajiwa, Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imemrejesha Michael Wambura kugombea urais wa Simba baada ya vikao vya siku mbili kujadili rufaa yake dhidi ya kuenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo, uamuzi uliofanywa kwa kupiga kura na hivyo kumpitisha kwa kura 3-2.
Hata hivyo, Wambura bado anasubiri hatima yake kwenye Kamati ya Maadili ya TFF ambako amefunguliwa mashtaka ya kukiuka katiba ya Simba kwa kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe Kamati ya Utendaji na kukosa maadili ya uongozi kwa sababu alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF na pia sio mwajibikaji.
Mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya TFF, Julius Lugaziya alisema: “Baada ya kupitia rufani na kusikiliza pande zote, kamati imehitimisha uamuzi kwa kuridhishwa na maamuzi yaliyofanywa na kamati ya utendaji Mei 5, 2010 ya kumsimamisha mwekewa pingamizi kuwa bado yana nguvu za kisheria kwa sababu hakuna maamuzi ya mkutano mkuu ya kubatilisha hatua hiyo.”
“Mwanachama ambaye amesimamishwa uanachama hana haki ya kushiriki katika shuguli za Simba kwa mujibu wa ibara ya 12 (3) ya katiba ya Simba ya mwaka 2010 na ibara ya 12 (3) ya katiba ya Simba ya mwaka 2014.
“Katika kujadili hoja hii Kamati ilijiuliza, kama kweli mrufani amesimamishwa, kamati ilipokea ushahidi tangu alipotangazwa kusimamishwa Wambura na kuonekana hajawahi kuchukuliwa kama mtu aliyesimamishwa.”
Mwananchi

No comments: