ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 17, 2014

ZILIZOTUFIKIA HIVI PUNDE,Shambolic lengine lakumba Mpeketoni


Shambulizi lengine limetokea katika eneo la Mpeketoni karibu na Lamu , pwani ya Kenya na kusababisha vifo vya watu 10.
Shambulizi la leo limetokea siku moja tu
baada ya Al Shabaab kukiri kufanya mashambulizi yaliyowaua watu 50 Jumatatu.
Polisi wanasema kuwa washambuliaji hao walivamia kijiji kimoja usiku kucha.
Kundi la Al Shabaab lilikiri kufanya mashambulizi hayo na kuambia shirika la habari la Reuters kuwa operesheni yao ya mashambulizi itaendelea nchini Kenya.
Takriban watu 50 waliuawa katika mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.
Taarifa zaidi zitakujia hivi punde
BBC

No comments: