
“Ni wakati mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kazi yangu ya ukocha na
siku mbaya zaidi katika maisha yangu ya soka. Lakini maisha yanaendelea.
Nani anawajibika kwa
matokeo haya? Ni mimi, ni mimi. Lawama za matokeo
haya mabaya zinaweza kutuhusisha wote, lakini mtu aliyeamua timu ya
kucheza na mbinu nilikuwa mimi.
Lilikuwa chaguo langu. Tulijitahidi kufanya kila tuwezalo, tulicheza kwa kiwango chetu cha mwisho-lakini
tumeishia dhidi ya timu kubwa ya Ujerumani. Hatukukata tamaa na kurudi
nyuma. Tuliparaganyika na kupaniki baada ya kufungwa bao la kwanza na
kila kitu kiliharibikia hapo. Hata Ujerumani hawawezi kuelezea
ilitokeaje-lakini ni kwasababu ya ujuzi wao na unatakiwa kuheshimu hilo.
Tunatakiwa kujifunza jinsi ya kukabiliana nalo. Ujumbe wangu kwa watu
wa Brazil ni huu. Tafadhali watusamehe kwa kiwango hiki. Ninaomba radhi
kwasababu hatujaweza kufika fainali na tutajitahidi kushinda mechi ya
nafasi ya tatu. Bado tuna sababu ya kucheza.”
No comments:
Post a Comment