ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 8, 2014

ANGALIA PICHA BIRTHDAY YA MAMA YAKE DIAMOND AMZAWADIA GARI LA MILIONI 38..



Ingawa Diamond hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mama yake. 
Ni Toyota Lexus New Model ambapo Babu Tale amesema imegaharimi milioni 38.1 ambapomilioni 35 imetumika kulinunulia gari hilo mpaka kuingia Tanzania na Milion 3.1 imetumika kulipamba na kuweka Music System pamoja na seat Cover.

Zawadi hii ameitoa Diamond kwa mama yake kama zawadi kwa ajili ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa mama yake ambaye amesema ametimiza miaka 55, mama yake amesema hakutegemea zawadi hii na anamuombea mwanae kwa Mungu afanikiwe zaidi.
Baada ya kufuturu Meneja wa Diamond Babu Tale alitangaza utaratibu wa kuzindua kwanza video mbili za Diamond kwa watu waliokuwepo hapo kisha utaratibu mwingine ukaendelea ikiwemo kumuimbia mama yake Diamond kisha kukabidhiwa gari yake

5 comments:

Anonymous said...

Y'ALL BE TRYING TO MUCH, its not a must kuandika kingereza when what your writtin doesnt make sence, its managers? what kind of english is that mnatutia aibu

Anonymous said...

Hata na wewe unatia aibu...kwa Kiswahili pia kiingereza chako. Hatusemi "kingereza" bali "kiingereza". Pia uliposema "...your..." inaelekea ulitaka kusema "...you are...". Halafu "...sence..." huandikwa "...sense...". Upo hapo ndugu anonymous...?

Anonymous said...

Diamond hapa tuu ndiyo unapotukweza kina mama! Wacha waseme kijana PEPO utaiona kwa kumtunza mama aliyekuzaa ndiyo maana wanakusingizia uchawi. Huu ndo uchawi wa DIAMOND. Mungu atakubariki tuu kama utaonyesha heshima na mapenzi kwa wazazi wako bila kujali kuwa unapesa kiasi gani. Just a humble loving young men! Mungu ataendelea kukufungulia mambo mengi makubwa just continue doing the right things. TUPENDE WAZAZI WETU...NA TUWATUNZE

Anonymous said...

na wewe pia what kind of english is that unajaribu kuwakosoa wenzako na wewe yale yale blululaaaaaa wa kupindukiza .spelling ya writing aunandika writtin, na ni past tense unatakiwa ungeandika wrote siyo writtin na y'all ndo kizungu gani hicho cha kiafrica america cha mitaani ukienda college ukiandika hivyo hupasi unatoka na mayai zero zero.
you too you dont make a sense unalivyojaribu kuwakosoa wenzako ndo maana unaambiwa nyani halioni....ku..nd.le...

umetia kinyaa na aibu kubwa wewe kuliko wenzako because you try to correct them wakati wewe hukijui hata kukiandika hicho kizungu... ovyoooo mtuzima ovyoooo

Anonymous said...

wema you are trying all you best my dear kujipendekeza kwa mama mkwe make sure this time for really unaolewa utulizane uzae watoto wako si kujipendekeza kila siku mwisho wa siku ukatupwa kama taka taka you have to grow up and be smart my dear.

ushauri wa bure anaye kutakia la kheiri fan wako. belgium