ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 19, 2014

Chadema yapasuka Kigoma

Bendera za Chadema

Kigoma. Viongozi watatu wa Chadema mkoani Kigoma, wametangaza kujitoa katika chama hicho kwa madai hakina demokrasia.
Viongozi waliojitoa ni Kasisiko Ramadhani ambaye alikuwa Mwenyekiti Mkoa, Msafiri Wamalwa Katibu Mkoa na Malunga Simba, Katibu Bawacha.
Mwenyekiti wa chama hicho Kasisiko Ramadhani ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa baraza la wazee taifa alisema, uamuzi huo ameutoa kutokana na migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza hasa kwa kutotenda haki kwa wanachama wake.
Kasisiko alisema awali chama hicho kilikuwa kinaheshimu demokrasia, lakini sasa kinatumia ubabe na kutoa uamuzi usio wa busara.
Alisema, chama hicho kimeanza kukiuka katiba kwa kuwa hakuna mahali palipoandikwa masharti ya mwanachama kugombea nafasi yoyoye na kwamba mwanachama Zitto Kabwe alitolewa katika Chama hicho kwa kutaka kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa.
Kwa upande wake katibu wa chama hicho Mkoa Msafiri wa Malwa, alisema sababu kubwa ya kujitoa katika chama hicho ni kukuza demokrasia ya nchi kutokana na kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa vyama vingi ni pamoja na kukuza demokrasia.
Naye Malunga Simba ambaye ni katibu Bawacha Mkoa alisema amehama chama hicho kwa moyo mmoja kutokana na chama hicho kuwa na masilahi ya watu wa chache ikiwa ni pamoja na kutotenda haki kwa wanachama wake.
Mwanachi

No comments: