Aliyekuwa kiungo wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Athumani Iddi Chuji
Aliyekuwa kiungo wa Yanga na timu ya Taifa (Taifa Stars), Athumani Iddi ‘Chuji’ amesajiliwa kwa mkataba wa muda mfupi wa miezi sita na mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, Azam, imefahamika jana jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo bado uongozi wa Azam umekanusha kumsajili kiungo huyo wa zamani wa Polisi Dodoma na Simba na kusema kwamba ameomba kufanya mazoezi na kikosi hiko.
Chuji jana asubuhi alianza rasmi mazoezi na wachezaji wa Azam na alionekana kushirikiana vyema na nyota wa timu hiyo inayonolewa na kocha Mcameroon Joseph Omog.
Kocha huyo aliliambia gazeti hili kwanza ameridhika na kiwango cha Chuji na kutokana na uzoefu alionao ataisaidia Azam katika msimu ujao na mashindano ya kimataifa watakayoshiriki.
Omog alisema kwamba katika mashindano ya kimataifa, wachezaji wazoefu ni muhimu kwa sababu wanajua mbinu mbalimbali wanapokuwa ndani ya uwanja na kuwasaidia chipukizi kupambana na changamoto.
"Wachezaji wazoefu ni mali na wana mchango sana katika mashindano ya kimataifa," alisema Omog jana asubuhi.
Katibu Mkuu wa Azam, Nassor Idrissa, alisema jana kuwa bado wako katika mazungumzo na Chuji na atakayeamua ni kocha mkuu baada ya kuridhishwa na kiwango chake.
Naye Afisa Habari za Azam, Jaffer Iddi, alisema kwamba bado Chuji hajasaini mkataba wowote na timu hiyo na ameruhisiwa kujinoa kama alivyoomba.
"Watu wanauliza mbona amevaa na jezi mazoezini, hilo ni jambo la kawaida hata wachezaji wa Simba na Yanga wanapokwenda kucheza ndondo, huvaa jezi za timu husika wanayoichezea," Idd alisema.
Ili kujiweka 'fiti' na kabla ya Yanga haijatangaza kumtema, alikuwa akijifua ufukweni na baadaye alihamia gym ili kujiweka imara.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment