Advertisements

Wednesday, July 23, 2014

DIAMOND MKUBWA HAKOSEI, ANASAHAU TU!


KWAKO,

Nasibu Abdul ‘Diamond’. Bila shaka utakuwa mzima wa afya njema mdogo wangu. Mimi nipo poa, naendelea na mchakamchaka wa maisha kama kawaida. Leo nimekukumbuka kwa barua.Nikuambie ukweli, barua hii naandika kwa hisia kali sana, nikiwa na lengo la kukushauri jambo jema ambalo litayafanya maisha yako yaendelee kuwa mazuri bila vikwazo.

Kuna kitu kinaendelea ambacho ukikitazama kwa juujuu unaweza kuona ni kidogo lakini ukitafakari kwa kina utaona namna lilivyo na umuhimu mkubwa katika maisha yako.Ni kuhusu baba yako mzazi, mzee Abdul Jumaa. Sitaki kuingilia maisha yako, si lengo langu kukupangia namna ya kuishi lakini nalazimika kukushauri kwa upendo kabisa, ushauri ambao una uhuru wa kuupokea au kuuacha.

Nimefanya hivyo mara nyingi kwako kuhusiana na mambo mbalimbali, ndani na nje ya muziki wako wa Bongo Fleva. Nakuomba utulize moyo.Usishangazwe na namna mambo yako binafsi ya kifamilia yanavyoingiliwa kwa sasa. Hiyo ni kwa sababu ya ustaa wako. Wewe ni mtu wa jamii.

Watu wanajitazama kupitia kwako.Inaelezwa kuwa baba yako kwa sasa ni mgonjwa na hana msaada wa matibabu. Maelezo yanasema kuwa, kwa muda mrefu huna maelewano na mzazi wako huyo.

Sitaki kuingia ndani sana, wala sihitaji kujua sababu ya kutokuwa na maelewano na mzazi wako lakini kwa uchunguzi niliofanya, inaonyesha kuwa, mzee wako anakupenda kama mwanaye na yupo tayari kushirikiana na wewe.

Kuna wakati nilimsikia mzee akisema, hahitaji fedha zako (akimaanisha si kwamba anataka kuchukua utajiri wako) bali anatamani uhusiano wako na yeye, kama mtu na baba yake urudi!Hiyo ni busara ya hali ya juu. Diamond nataka kukuambia jambo moja mdogo wangu, zipo baraka nyingi sana kupitia kwa wazazi.

Kwa bahati mbaya, wazee wamepewa nguvu ya kuamua maisha ya watoto wao.Mzazi akikasirika anaweza kutamka neno baya likakufika. Amini usiamini, ipo hivyo na haiwezi kubadilika.

Hata vitabu vitakatifu vinaeleza hivyo waziwazi.Kuna mahali kwenye maandiko kumeandikwa: Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.Andiko hilo pekee linatosha kutuongoza kuwaheshimu wazazi kwa kila namna.

Inawezekana kuna mambo ambayo mzee wako ameyafanya yakawa kikwazo kwako, isiwe tabu. Waswahili wanasema: Mkubwa hakosei, anasahau tu!Chondechonde mdogo wangu, rudisha uhusiano mwema na mzazi wako, baraka zitazidi na Mungu atakuongezea katika shughuli za mikono yako. Nitafurahi kama utaelewa na kuyafanyia kazi.Yuleyule,
Mkweli daima,
.....................
Joseph Shaluwa

GPL

3 comments:

Anonymous said...

Yaani umeacha kazi zako na kuandika haya:( Hivi mahusiano ya Diamond na baba yake yanatuhusu nini? UUnafahamu kilichowatenganisha? Diamond hakuzaliwa tajiri na ni Diamond pekee ndiyo a naefahamu ugomvi wake na baba yake..kwa kinadharia tusiomfahamu Diamond tunaona mapenzi yake ya dhati kwa mama yake..iweje amsahau baba? JIBU jepesi ni Kwamba huyu baba inawezekana hakushiriki kumlea Diamond..:( Nyakati zimebadilika na sisi t ubadilike....kama humlei mtoto ni kwa nini mtoto awe na wajibu wa kusumbuka na wewe anapokuwa mtu mzima? Mtoto anahitaji wazazi ktk kipindi cha utoto...kikishapita kipindi cha utoto akawa ameishi bila ya uwepo wa baba inakuwa ni uchaguzi wake kama huyo baba atajitokeza kuomba msamaha. .lakini hatuna haki kumkosoa mtu anaekataa mrejesho wa mahusiano Kati ya baba na mwana..Tubadilike! Watoto tunaowazaa wanatuhitaji sana kuliko kipindi chochote maishani mwao wanapokuwa wadogo kwa mapenzi, chakula na sehemu salama ya Kuishi! ! DUNIA YA KUZAA na kusepa IMEKWISHA ..UKISEPA usimtafute mtoto anapokuwa hakuhitaji tena..tuachane na unafiki...tuwe wa kweli hata mungu amemlaani mzazi anaetekeleza kiumbe wake..unaweza kumsamehe kibinadamu lakini mahusiano siyo lazima na wala DUNIA haitokushangaa..hapa Marekani kuna Mastaa matajiri kikweli kweli lakini hawataki kusikia kuhusu baba na inaeleweka..kama hukunitaka wakati nilipokuhitaji zaidi ni kwa nini uwe kwenye maisha yangu kipindi ambacho sikuhitaji?

Anonymous said...

I love the statement

Anonymous said...

Halo watu wote, jina langu ni Marvelyn Larry. Kwa muda mrefu, mume wangu alikuwa akiishi katika ghorofa nyingine kutokana na shinikizo la kazi na tulifurahi sana pamoja ingawa alikaa mbali nasi kwa miezi kadhaa. Sikujua mwenzangu wa kazi tayari alikuwa na uhusiano naye jambo ambalo lilimfanya mume wangu anipe talaka bila kutarajia. Nilijua kuna kitu kibaya kwa sababu hatukuwahi kupigana au kubishana kiasi hicho ili kumfanya aondoke. Nilikuwa na kiwewe na natafuta msaada wa kukabiliana na hali hiyo iliyonipeleka kwa DR DAWN kutokana na sifa walizomwagiwa na watu mtandaoni. Tulizungumza kwa kirefu na aliniambia kila kitu nilichohitaji kujua kuhusu kile kilichotokea na utaratibu unaofaa wa kurekebisha matatizo. Alitimiza ahadi zake na kumrudisha mume wangu kwangu na mchakato wa talaka ukafutwa. Sasa mume wangu amerudi nyumbani kwetu na tuna furaha pamoja. Inashangaza sana jinsi watu wanaweza kusaidia watu wengine wakati wanahitaji. Anaweza kukusaidia pia. Mtumie tu ujumbe kupitia WhatsApp: +2349046229159
Barua pepe: dawnacuna314@gmail.com