ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 15, 2014

ERICA LULAKWA AICHANGIA JENGA TANZANIA FOUNDATION DVD 120, MWIGULU AIFAGILIA

Naibu Waziri wa Edha (S) Mhe.Mwigulu Nchemba akutana na Kiongozi wa JENGA Tanzania Foundation Bwana Nassor Basalama mjini New York, ambapo wamejadili suala la kusaidia wanawake na watoto wasiojiweza Tanzania.
Mwimbaji maarufu anayeishi California Erica Lulakwa, 
Amechangia katika JENGA Tanzania Foundation jumla ya DVD 120 za documentary ya HIV aliyoifanya Tanzania. Ili ziuzwe na pesa yote itakayo patikana, iende kwenye mfuko wa JENGA. Msaada huu ameutoa kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za kusaidia watoto wasiojiweza katika elimu na afya ya kinamama. Mwanadada huyu pia ameguswa sana na uchunguzi wa vipimo vya kisasa vinavyo fanyiwa utafiti juu ya uthibati wake katika kugundua malaria unaofanywa na Dr. Habib na Dr.Diwani chini ya JENGA TANZANIA FOUNDATION. 
Mkurugenzi wa JENGA, Bwana Nassor Basalama, anaamini vipimo hivi vikithibitika kuwa vinafaa, itakuwa ni ukwamuzi mkubwa wa kadhia ya gonjwa hili ambalo limekuwa ni usumbua na kero la muda mrefu kwa Watanzania. Pia Bwana Nassor anaamini mradi huu utakuwa umekamilika na hata kuwafikia walengwa mnamo mwezi wa November.

No comments: