Mimi ni Mtanzania ninaeishi nchini Uingereza na siku zote nimekua nikifuatilia huu uchaguzi wa Jumuya ya Watanzania DMV na kuona umekuwa wa mwamuko mkubwa na upinzani mkali kuliko hata uchaguzi wa Wabunge Tanzania na nadhani siko peko yangu ninayejiuliza maswali kama hayo kwamba huo uongozi wa Jumuiya wa DMV ni kitu gani kikubwa wanachopigania sidhani uongozi tu wa kujitolea kuwaongoza Watanzania wenzako ndio unaoweza kuleta malumbano yote haya.
Mimi naitwa Zeno Mkandawile ninaishi hapa Uingereza sasa kwa miaka nane na nimekua nikiufuatilia huu uchaguzi wa DMV tangia ule wa miaka miwili iliyopita wakati Rais wa sasa Iddi Sandaly alipokua akigombea na dada Loveness Mamuya mambo yalivyokua yakiendeshwa kwa wagombea kuweka sera zao kwenye mitandao na hata kurekodi video zao za kujinadi na kutengeza vipeperushi vyenye picha zao za kuomba kura kwa Watanzania wa huko DMV.
Mwaka huu naona uchaguzi wenu wa DMV umezidi kuwa moto zaidi kwa kila upande kujitangaza na kuweka mikakati ya nini watakachoifanyia jumuiya yao na kila upande kutetea sera zake na wengine kutoleana comment kali kwa mimi uchaguzi huu naona umeenda next level kitu ambacho hata uchaguzi wa Wabunge Tanzania sijawahi kukiona mpaka Watanzania tulio nje ya DMV tunajiuliza hii kweli ni kutaka kuongoza tu au kuna kitu DMV? Kama kuna mtu anaweza kunieleza ni kitu gani hasa kinachongombaniwa namna hii, kwa sababu ukifuatili chaguzi zingine za Watanzania ndani na nje ya Tanzania kwenye jumuiya mbalimbali haijawahi tokea kama DMV. Tuambieni Watanzania wenzetu wa DMV nini mnachogommbea kwenye chaguzi zenu na kama kina faida na sisi tulionje ya DMV tuweze kukusanya nguvu za kuamia huko.
Pia napenda kutoa shukurani kwa timu ya Vijimambo kuamua kuzipiga chini comment zote kwenye uchaguzi huu kitu kilichosaidia kutuliza muunkali na ushabiki uliokua ukiendelea kila upande mpaka kuonekana kuleta uhasama wa pande zote.
Kitu kingine naomba Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kama unaweza kuwaita wagombea wote na kuwakalisha chini na kuwaelimisha jinsi ya kuendesha uchaguzi wenye amani na utulivu.
Mwisho ninawatakia uchaguzi mwema ulioja upendo na yeyote atakayechagulia akubalike pande zote na apewe ushirikiano kwani wote ni Watanzania na daima nchini nyingi hutuonea wivu kwa mshikamno wetu.
Asante ni hayo tu kwa leo.
6 comments:
Hata siamini kama ni wingereza,wewe ni mtanzania wa hapa dmv
Hii inaonyesha kuwa dmv inapenda na kuheshimu watu wa dmv ndio maana watu wako so involved.Hakuna magovi
Wewe dada yangu pole sana ukisikia mtu yuko Marekani ujui ni DMV, if you can't make it in DMV you will never make it anywhere? hapa ndio jikoni...siyo kwa waTanzania tu hata wamerekani. Ukiacha utani hapa pana kila aina ya opportunity. Serikali yote ipo hapa. Ujanja ni kuwahi tu..Si sawa na Reading ya Uingereza, hapa ni Mission babkubwa all the movers and shakers wako hapa...
Mdau wa UK huu uongozi ni kazi ya kujitolea, wala hakuna mishahara. Kwa mtazamo wangu na uzoefu wa kuishi hapa DMV kwa karibu miaka 12 sasa, wagombea hufanya hivyo kwa mioyo yao tu ya kupenda kuwatumiakia wenzao na kuboresha 'resume' au (CV) zao.
Ndugu hakuna mishahara wala kipato utakacho pata, USA kunakitu kinaitwa kujitolea , kama hauku jitolea kwa public hata kama umepata masters utakua na utata kweye kuajiliwa, pia ukiona hivi ni neema za watu wa DMV baada ya pesa ni tittle pamoja na heshima kwa kazi nzuri , haya ni baadhi ya watu wanaoyotafuta, mishahara itakuja baada ya kazi inzuri
All you get is to sit on the same table with Hon. President J K and other leaders when they visit DC. Lol, and to clap hands and agree with whatever they say. Kidumu Chama cha Mapinduzi.
Post a Comment