SAKATA la wafanyakazi wa
ndani kunyanyaswa na mabosi wao limeingia katika sura ya kipekee, safari
hii mabosi wamegeukwa ambapo mmoja amedaiwa kuuawa na hausigeli wake
aliyetajwa kwa jina la Valentina Karenge (17).
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya mfanyakazi huyo wa ndani
mkoani Singida kudaiwa kumuuua tajiri yake kwa kumchoma kisu sehemu ya
juu ya titi la kulia kwa madai ya kunyanyaswa naye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida (SACP) Geoffrey Kamwela alisema tukio hilo la aina yake lilijiri saa 10 alfajiri Juni 29, mwaka huu eneo la Sabasaba, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida.
Kamanda Kamwela alimtaja marehemu kuwa ni Pendo Justine Kiula (24) ambaye ni Karani wa Mahakama ya Wilaya ya Singida.
“Baada ya marehemu kuchomwa kisu na msichana wake huyo, alitoka nje
ya nyumba na kukimbilia kwa majirani kwa ajili ya kuomba msaada lakini
wakati majirani wakiwa katika harakati za kumpeleka hospitali, alianguka
chini na kufa papo hapo,” alisema Kamanda Kamwela.
Alisema baada ya polisi kuendesha msako kwa kushirikiana na raia wema hatimaye walifanikiwa kumkamata msichana huyo majira ya saa 8 mchana uliofuata maeneo ya Uwanja wa Ndege akiwa katika harakati za kutoroka.
Naye Naomi Abrahaman ambaye ni mpangaji mwenzake marehemu, alisema
kabla ya tukio hilo walikuwa pamoja jioni na kushiriki chakula cha jioni
na kisha wakaenda kulala.
Alisema ilipofika saa kumi kasoro usiku, alishituka kugongewa mlango na marehemu na alichokisikia akikizungumza ni; Kwa jina la Yesu nakufa, kwa jina la Yesu nakufa.’
“Alipiga mlango wangu kwa nguvu na damu zilikuwa zikimvuja, akaenda
kwenye chumba kingine cha mpangaji akapiga tena mlango huku akisema
jamani nisaidieni nakufa, kwa jina la Yesu nakufa, akaanguka.
“Nilipotoka chumbani, nilimkuta ameanguka chini huku akiwa
ameshikilia pale alipochomwa kisu huku damu zikiendelea kumtoka.”
Alisema mpangaji huyo.
Akaendelea: “Kumbe mtuhumiwa alimchoma kisu wakati chumb ani
kukiwa na giza, baada ya kufanya tukio hilo alikimbia nasi tukawa
tunaogopa kuingia chumbani kwa kuhofia pengine kunaweza kukawepo mtu
aliyejibanza ndani ya chumba hicho.”
Marehemu alizikwa Julai 2, mkoani Singida. Ameacha mtoto mmoja.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake. Amina.
CHANZO:GPL
2 comments:
Bongo kiukweli mahouse girl wengi wananyanyaswa sana.
Kibao kinawageukia
Post a Comment