Mkazi wa mtaa wa Msamvu B kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro, Rehema Juma akiwa na majeraha baada ya kushambuliwa kwa wembe na mwanamke mwenzake aliyemtuhumu kutembea na mume wake, mkoani Morogoro. Picha na Juma Mtanda.
Na Hamida Shariff, Morogoro.
Mkazi mmoja wa Mtaa wa Msamvu B mjini
hapa, Rehema Juma amekatwakatwa na wembe shavuni na mkononi kisha
kuvuliwa nguo na kupigwa na jirani yake akimtuhumiwa kutembea na mumewe.
Tukio hilo lilitokea
Jumamosi iliyopita mnamo saa 11:00. Mwanamke huyo alidai kuwa kabla ya kujeruhiwa aliitwa na jirani huyo na bila kujua alichoitiwa, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambako alifungiwa ndani.
Jumamosi iliyopita mnamo saa 11:00. Mwanamke huyo alidai kuwa kabla ya kujeruhiwa aliitwa na jirani huyo na bila kujua alichoitiwa, alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo ambako alifungiwa ndani.
Alisema akiwa ndani jirani huyo alimtuhumu kufanya mapenzi na mume wake na hata alipojaribu kukataa, alitishia kumuua.
“Kwa kuhofia kuuawa niliona nikubali tuhuma hizo
na aliniuliza ni mara ngapi nilifanya mapenzi na mume wake na kama
nilikuwa napewa pesa, hivyo nilikiri kufanya mapenzi mara mbili na kwa
mara ya kwanza alinipa Sh2,000 na mara ya pili alinipa Sh5, 000 na baada
ya hapo aliniachia na nikarudi nyumbani,” alidai Rehema.
Rehema aliendelea kudai kuwa siku hiyo mnamo saa
11:00 jioni binti wa mwanamke huyo alifika tena nyumbani kwake na
kumwambia anaitwa tena na mama yake.
Naye bila ya hofu alikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo na alipofika aliingizwa kwenye chumba kimoja ambacho alikuwamo mume wa mwanamke huyo na kuanza kumpiga, akamvua nguo na kumkatakata kwa kiwembe shavuni na mikononi.

Hapa akiongea na waandishi wa habari.
Alidai kuwa baadaye mwanamke huyo alianza kumpiga mume wake, lakini mwanaume huyo alichomoka na kukimbia na alipomkimbiza ndipo yeye alipopata nafasi ya kutoka nje akiwa amebaki hana nguo huku akichuruzika damu.

Aliporudi nyumbani kwake, Rehema alisema
aliongozana na mume wake Godfray Shichonge na ndugu zake wengine kwenda
polisi kutoa taarifa na baadaye walipewa PF3 kwenda kutibiwa.
Godfray Shichonge, ambaye ni mume wa Rehema alidai
kuwa tangu alipoanza kuishi na mkewe hajawahi kusikia taarifa zozote za
kufanya mapenzi nje ya ndoa yao na kuwa katika mtaa huo ni wageni na
hawana mazoea na mtu yeyote.
“Alipoitwa nyumbani kwa mama huyu na kufanyiwa
ukatili aliniacha nyumbani nikiwa nimepumzika na kabla ya kuondoka
aliniaga na nikadhani kuwa ni masuala ya kawaida ya kina mama. Ghafla
nilishtuka usingizini kutokana na kilio cha mke wangu aliyerudishwa
nyumbani akiwa anavuja damu na akiwa amevuliwa nguo zote,” alisema
Shichonge.
Alisema kitendo alichofanyiwa mke wake ni
udhalilishaji kwani hata kama mwanamke huyo alikuwa akimtuhumu kufanya
mapenzi na mume wake alipaswa kufuata sheria na siyo kumjeruhi kwa
kumkata kwa viwembe na kumvua nguo.
Mjumbe wa mtaa huo, Dimoso Frances alisema baada
ya mwanamke huyo kumkatakata mwenzake kwa viwembe, alikwenda nyumbani
kwa mjumbe huyo na kuomba asamehewe kwani alifanya hivyo kutokana na
hasira.
Dimoso alidai kuwa kutokana na hali ya majeruhi kuwa mbaya, hakuweza kutoa uamuzi wowote na hivyo aliamua kufuatilia taarifa hizo polisi ambako aliambiwa kuwa tayari kesi ya kujeruhi ilishafunguliwa kwa jalada namba MORO/IR/4009/2014.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tayari kesi ilishafunguliwa na mtuhumiwa amekamatwa akiendelea kuhojiwa zaidi.
Kamanda Paulo alisema baada ya mahojiano hayo na uchunguzi utakapokamilika, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakaman
No comments:
Post a Comment