ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 18, 2014

Jeshi la ardhini la Israel laingia Gaza


Israel imeanzisha operesheni ya nchi kavu pamoja na mashambulizi ya anga na baharini dhidi ya vuguvugu la kupigania uhuruwa palestina Hamas katika ukanda wa Gaza.

Katika kipindi cha siku kumi zilizopita zaidi ya wapalestina mia mbili wameuwawa katika mashambulizi ya anga yaliyotekelezwa na Israel na Muisraeli mmoja aliuwawa katika mashambulizi ya mizinga ya roketi kutoka Gaza.

Oparesheni hiyo ya kupeleka majeshi ya ardhini imenza usiku, ni operation kubwa kufanywa katika kipindi cha miezi mitano.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema lengo ni kuharibu kabisa miundo mbinu na silaha zinazotumiwa na vuguvugu la Hamas kuishambulia Israel.

Vifaru karibu kumi vimeshuhudiwa vikielekezwa Gaza huku mashambulio ya angani na majini yakiendelea, ripoti ambazo hazijathibitishwa zinasema huenda hata hospitali zimegwa na mizinga.

Watu zaidi ya 3 wamefariki katika duru hii ya mapigano mbali na wale zaidi ya 200 waliofariki awali.

Kundi la Hamas limesema watajibu oparesheni hiyo vilivyo lakini Israel inasema Hamas watapewa kipigo cha kudumu na kitakachowasambaratisha kabisa.

Israel imewaita maelfu ya wanajeshi wake wa akiba kuweka nguvu zaidi katika operation hiyo.

Jana jamii ya kimataifa ilikuwa na matumaini makubwa kwamba huenda kukawa na usitishwaji mapigano wa kudumu baada pande zote mbili kukubali mapendekezo ya kusitisha mapigano kwa mda wa saa 5 za kuruhusu huduma za kibinadamu.

BBC

No comments: