Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akizungumza na Jaji Chang-ho Chung, Mgombea wa Nafasi ya Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutoka Jamhuri ya Korea ambaye alimtembelea Ofisini kweke tarehe 11 Julai, 2014. Jaji Chang-ho Chung ambaye kwa sasa ni Jaji wa Kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa katika Chemba Maalum za Mahakama nchini Cambodia ni mmoja wa Wagombea wanaowania nafasi sita za Majaji katika Mahakama ya ICC ambao uchaguzi wao utafanyika Mjini New York, Marekani mwezi Desemba 2014 wakati wa Kikao cha 13 cha Nchi Wanachama waliosaini Mkataba wa Rome ulioanzisha ICC.
Jaji Chang-ho Chung akimweleza jambo Katibu Mkuu.
Jaji Chang-ho Chung akizungumza huku akisikilizwa na Katibu Mkuu na wajumbe wengine akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (wa kwanza kulia)
Jaji Chang-ho Chung akisaini Kitabu cha Wageni huku Bw. Haule akishuhudia.
Balozi Kasyanju na Afisa kutoka katika Kitengo cha Sheria, Bw. Abdallah Mtibora wakiwa kwenye kikao cha Jaji Chang-ho Chung na Katibu Mkuu Haule (hawapo pichani).
Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.
No comments:
Post a Comment