Na Mohab Dominick
Shinyanga
July 25,2014
Kikongwe sayi (75)mkazi wa kijiji cha mwagata kata ya mwamalili manispa ya shinyanga ameuwa kikatili kwa kukatwa na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake na kufariki dunia.
Kamanda wa polis mkoa wa shinyanga justu kamugisha amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa tano za usiku kwa kikongwe huyo .
Akifafanua zaidi kamanda alisema kuwa wakati kikongwe huyo amelala na wajukuu wake wawili ghafla alivamiwa na watu wawila ambao akuwafahamu na kumcharanga na mapanga.
.
Aidha kamanda alisema kuwa walimcharanga sehemu mbali mbali za mwili wake ikiwemo shingo ,mabenga ,ali ambayo ilipelekea mauti yake kikongwe huyo .joel machia (45)mkazi wa mwamalili anashikiliwa kwa tuhuma hizo na kwamba uchunguzi wa jambo hili unaendelea .
Kamanda justu pia amesema kuwa jeshi la polisi katika uchunguzi wa awali limebaini kuwa chazo cha ugomvi huo ni kugombea mashamba .
Aidha mkoa wa shinyanga umekuwa na matukio ya mara kwa mara ya ukatili wa vikongwe katika mkoa huo jambo ambalo linatia shaka maisha yao kwa mwezi huu ni kikongwe wa 4 tiali wamekwisha uawa kwa dhima hiyo ya mashamba na uchawi.
No comments:
Post a Comment