Kufanya mahafali ya pili kesho Julai 12
baadhi ya picha eneo la chuo hicho,
Maandalizi ya sehemu ya mahafali hayo hiyo kesho Julai 12.
ubao chuo
Chuo cha Kilimo na mifugo Kaole
Na Andrew Chale, BagamoyoCHUO cha Kilimo na Mifugo Kaole (Kaole College of agriculture (KCA), kesho Jumamosi Julai 12, kinatarajia kufanya mahafali yake ya pili chuoni hapo huku wahitimu 291, wakitarajiwa kutunukiwa vyeti mbalimbali.
Akizungumza mjini hapa, principle wa chuo hicho, Cuthbert Liwa alisema kuwa, tayari maandalizi yamekamilika na mahafali hayo yatafanyika kwenye viwanja vya chuo hiko.
“Jumla ya wahitimu 291, wanatarajiwa kuhitimu na kutunukiwa vyeti vyao. Kati ya hao, wahitimu 179, fani ya Kilimo na wahitimu 112, kwa fani ya Ufugaji” alisema Liwa.
Aidha, alisema mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, anatarajiwa kuwa Dr. Masuruli wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Aidha, aliwaomba watu mbalimbali kujumuika kwa pamoja kwenye mahafali hayo, chuoni hapo, Kaole, Bagamoyo. (the college is located in South-East Bagamoyo 3.5 km from Bagamoyo township in the premises of Kaole Secondary school. The centre is along the showers of the Indian Ocean).
No comments:
Post a Comment