ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, July 22, 2014

MAREKANI YASITISHA USAFIRI WA ANGA KUELEKEA TEL AVIV KWA SAA 24

Usafiri wa anga nchini Marekani umesitisha usafiri wa anga wa ndege za nchi hiyo zinazofanya safari zake kutoka nchini humo kuelekea Tel Avivi nchini Israeli kwa saa 24 kwa kuhofia usalama wa ndege hizo kutokana na makombora yanayoendelea kurushwa kati ya Israel na Palestina.

Mashirika ya ndege ya Marekani yanayofanya safari za anga nchini Israel ni Delta, United na US Airways.

Uamuzi huo umetokana na makombora yaliyoelekezwa kwenye uwanja wa ndge wa kimataifa wa Ben Gurion uliopo kwenye mji wa Tel Aviv. Wakati uamuzi huo unatolewa ndege ya shirika la ndege la Delta iliyoandoka asubuhi ya leo kutokea New York kuelekea Tel Aviv ilibidi ibadilishe njia na kuelekea Paris,  shirika la ndege la Israel ambao ndege zao zinaweza kujikinga na makombora hayo baada ya kujengea kifaa kinachoweza kubadili mwelekeo wa kombora hilo.

Mashirika mengine ya ndege yaliyositisha safari zake kuelekea Tel Aviv ni KLM , Air France na Lufthansa.

No comments: