ANGALIA LIVE NEWS

Friday, July 11, 2014

Mashabiki wa Ghana waomba kuhamia Brazil

Mashabiki hawa walienda Ghana kutazama kombe la dunia
Polisi nchini Brasil wamesema kuwa mashabiki 200 kutoka Ghana waliaokwenda nchini humo kutazama kombe la dunia wanataka waruhusiwe kuhamia nchini humo.
Waliingia nchini humo kwa kutumia viza za kitalii kwa lengo la kushabikia kombe la dunia
Afisa kutoka wizara ya haki nchini humo alisema kuwa japo wa-Ghana hao walitumia viza za kitalii kuingia Brazil, swala hilo halifai kutiliwa maanani katika uamuzi wa kuwaruhusu kuhamia nchini humo.
Wa-Ghana hao wanadai wao ni waislamu wanaokwepa migogoro ya kidini nchini kwao.
Sheria za Brasil zinaruhusu mahamiaji kufanya kazi nchini humo baada ya kujiandikisha rasmi.
Waliandikisha maombi yao kwenye mji wa Caxias do Sul, mojawapo ya miji iliyostawi zaidi nchini humo.

'Ghana ni nchi salama'
Ghana ilitimuliwa kutoka kombe la dunia Brazil katika wamu ya 16 bora
Madai haya yamepingwa na serikali ya Ghana ikisema kuwa nchi hiyo haukumbwi na migogoro yoyote ya kidini.
Serikali imesema Ghana ni mojawapo ya nchi salama na tulivu barani Afrika. Ubalozi wa Ghana nchini Brazil umetakiwa kuchunguza madai hayo.
Anavyoelezea Joao Guilherme Granja, ombi la uhamiaji haliwezi kutolewa katika ubalozi, bali wanaotafuta kuhamia nchi ngeni wanapaswa kuwa ndani ya nchi wanayokusudia kuhamia ili kutoa maombi hayo.
Aidha alisema kuwa kuna wahamiaji kutoka Syria wako katika hali hiyo hiyo nchini Brasil.
Wengi wa wahamiaji walio mji wa Caxias do Sul wamepewa makao na makanisa ya Katholiki.
'Zaidi ya watu elfu moja'
Kwa mujibu wa polisi wananchi wa Ghana elfu moja zaidi wanatarajiwa kutoa maombi ya kuhamia nchini Brasil wakitaka ruhusa ya kufanya kazi nchini humo.
Mkuu wa polisi Noerci da Silva Melo akiwa Caxias do Sul alisema, “Eneo la Serra Gaucha linajulikana kuwa na nafasi za kazi tele na kuvutia wafanyikazi kutoka nchi za kigeni.”
Aidha bwana Melo aliongezea kuwa kuna msangamo katika eneo hilo sasa, kwani upitapo njiani utaona wachuuzi kutoka Haiti na Senegal.
Eneo la Caxias do Sul liko kilomita elfu moja mia sita kutoka kaskazini mashariki mwa Brasil ambako Ghana ilishiriki kwenye michuano ya kombe la dunia.
Timu ya Ghana haikuponea mchujo baada ya kupoteza mechi mbili, dhidi ya Marekani na Portugal, na baadaye kutoka sare na Ujerumani.
BBC

No comments: