BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHI MAREKANI, MHE.
LIBERATA MULAMULA, ANAWAALIKA WATANZANIA KUTOKA KWENYE MAENEO YA DMV PAMOJA NA
MAJIMBO MENGINE HAPA MAREKANI, KUHUDHURIA MKUTANO MAALUM WA RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA, MHE. DR. JAKAYA KIKWETE, UTAKAOFANYIKA TAREHE 2 AGOSTI,
2014 KATIKA HOTELI YA MARRIOT, 1221 22ND ST NW, WASHINGTON DC 20037,
KUANZIA SAA 12.00 KAMILI JIONI.
KWA WALE WATAKAOITIKIA MWALIKO HUU NA KUTAKA KUHUDHURI, WANAOMBWA
NA KUHIMIZWA KUFANYA YAFUATAYO:
A.
KUJIANDIKISHA MAJINA KWA VIONGOZI WAO WA JUMUIYA, MWISHO NI SIKU YA
IJUMAA TAREHE 1 AGOSTI, 2014, AMBAPO VIONGOZI HAO WATAWASILISHA MAJINA HAYO
SIKU HIYO IFIKAPO SAA 6.00 MCHANA, KWA NJIA WALIOKWISHAELEKEZWA.
B.
KILA MSHIRIKI ATAPASWA KUWAHI SAA MOJA NA NUSU KABLA YA MKUTANO
KUANZA, ILI KUJIPA FURSA YA KUTOSHA KUKAMILISHA TARATIBU ZA KUINGIA UKUMBINI.
C.
WATU WOTE WATATAKIWA KUWA WAMEKETI UKUMBINI IFIKAPO SAA 11.40
JIONI. HAKUNA MTU ATAKAYERUHUSIWA KUINGIA TENA UKUMBINI BAADA YA MUDA HUO.
D.
KILA MSHIRIKI ANAPASWA KUWA NA HATI YAKE YA KUSAFIRIA AU/NA
KITAMBULISHO HALALI CHENYE PICHA YAKE KUTOKANA NA TARATIBU ZA KIUSALAMA.
KARIBUNI KATIKA KIKAO HICHO, FURSA MUHIMU
AMBAYO KWA MARA NYINGINE MHE. RAIS AMETUPAPITIA TANZANIA DIASPORA
9 comments:
This is a three day notice!??
Hatuna viongozi wa jumuiya sasa hivi
"This is a three day notice!??" Look here u have a choice. Don't start a blame game - a la Bongo! You have been given an opportunity to meet and converse with your President. If it doesn't look good to you, u are not compelled to take it. Shut up and go on with your life!
Kwa hiyo ulitaka 30 days notice kwani election ???! Tuondolee umbururaaa
Wewe unayesema hatuna viongozi haupo kwenye Jumuiya yetu hapa DMV. Viongozi tunao until Agosti 9 ndipo tutapata wapya. HUTAKI USIJIANDIKISHE NA UKAE HOME, MSITUCHAFULIE MJI WETU..
RAIS, MAKAMU, KATIBU NA MWEKA HAZINA MIMI NISHAJIANDIKISHA NA NINTAKUJA ASIYEWATAMBUA ALALE NYUMBANI.
I hope we aren't forgetting that this is The Embassy of the United Republic of Tanzania in the "United States". DMV is only a small part of the US.
"AMETUPAPITIA" ni kitu gani? Au siku hizi nimesahau Kiswahili?. Mnaoandika matangazo lazima mzingatie Kiswahili sahihi ambacho hakina makosa.
Na wale mnaokwenda kuchapisha mafulana yenu na maneno ya kutaka ugomvi myaache majumbani kwenu. Bado hatujapona vidonda ya aibu ya wanaume waliovaa mafulana wakijidai kudai TANGANYIKA siku ya muungano mbele ya wageni na watanzania wengine waliokuja kutusupport, we are here in the kitchen let us all show respect to our leaders na balozi wetu anayetupenda na kutuheshimu let us all give her that respect kama una issue zako mtafute she is always available kutusikiliza na yeye atapeleka ujumbe kunakohusika no need ya kusubiri hadi siku ya heshima ya sherehe za kitaifa au wageni wakiwepo ndo tunaonyesha how immature we are... WANA DMV TUWAKARIBISHE VIONGOZI WETU NA WAGENI WETU KWA HESHIMA NA TAADHIMA NA TUONYESHE TOFAUTI KUWA ANGALAU KUKAA HUKU MAJUU TUMEELIMIKA ZAIDI NA TUNA USTAARABU.
Tatizo maswali yote uwa wameshayapanga na waulizaji huandaliwa mapema. Maswali yenyewe Hawa ni utumbo mtupu.. Hata mtoto wa chekechea anaweza kuuliza swali la maana.
Post a Comment