Watanzania wote mliosoma habari za uzushi kuwa Mimi ni mbaguzi wa Dini,
habari hizi zimekuwa zikisambazwa Katika mitandao tofauti ya simu, Jamii forum
na Facebook na baadhi ya wagombea wa uongozi hapa DMV. Simpigii debe mgombea
uongozi yeyote kwani mimi ni Katibu wa Tume ya uchaguzi hapa DMV na nina haki
ya kukanusha habari hizi zisizo za ukweli na zenye nia ya kunichafulia
mahusiano niliyoyajenga na Watanzania wenye Imani ya dini tofauti tangu
nilipokuja nchi hii kama mtoto wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani
Mheshimiwa Balozi Mustafa Nyang’anyi. Kama familia tumekuwa na ushirikiano na
Watanzania wa Imani za dini zote kwa kipindi chote mzazi wangu alipokuwa hapa
kuanzia mwaka 1995 to 2002 kwani shughuli zote za kijumuiya zilikuwa
zikifanyika nyumbani kwa balozi na hapakuwa na ubaguzi wowote wa kidini na wale
mliokuwepo miaka hiyo mtakubaliana nami na nikaendelea na ushirikiano huo hadi
leo hii. Kwa wale wasionifahamu haya ndiyo malezi niliyopata kutoka kwa wazazi
wangu.
MCHANGO WANGU KWA JUMUIYA YETU HAPA
MAREKANI
1. Nimekuwa Mwanakamati wa jumuiya ya watanzania
tangu Jumuiya hii ifufuke mwaka 2012. Nimefanya kazi na viongozi wa ngazi zote,
kuanzia Bodi, na Executives. (Rais,
Makamu wa Rais, Katibu na Mweka Hazina) ambao majority ni wakristo.
2. Nilikuwa katibu wa Kamati ya maandalizi ya
mkutano wa DICOTA hapa Washington DC ambapo sherehe hizi ziliunganika na
sherehe za miaka 50 ya UHURU wa Tanzania na tulikuwa waislamu 2 katika Kamati
ya WATU 15. Tulishirikiana na uongozi wa juu wa DICOTA na Mheshimiwa Balozi
Mwanaidi Maajar na maafisa wengi wa ubalozi kufanikisha maandalizi ya sherehe
hizi na mkutano ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
alikuwa Mgeni rasmi.
3. Katibu wa Kamati ya maandalizi ya matamasha
ya vijimambo na katika vikao vyetu mimi Ndiyo niliyependekeza kumwalika Rais
nmstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa Wajumbe na wakaafiki pendekezo hilo. Kamati hii
inaongozwa na Baraka Daudi na mimi ni mwanamke pekee na tupo waislamu watatu.
Na nimefanya kazi kwa Karibu na maafisa wa ubalozi, Wahadhiri wa lugha ya
Kiswahili na wajasiriamali wa hapa Marekani wa Imani tofauti katika kufanikisha
Tamasha la vijimambo mwaka jana na tupo tunatayarisha tamasha lingine mwaka huu
na wengi mmeishaona matangazo.
4. Mratibu Ms. Tanzania USA pageant. Nimefanya
kazi kwa Karibu na founder mama Winny Casey kuandaa haya maonyesho kwa mara ya
kwanza hapa Marekani. Ni muislamu pekee katika Kamati yote na nimeshirikiana na
mabinti zetu walioshiriki kwa Mara ya kwanza, Wanakamati wasio watanzania na
wasio waislamu. Tuliwapokea toka states mbalimbali na Mimi niliwahost
wasichana wote waliotoka out of state na
wa hapa kuwatoa usiku kwenda kuona mji wetu na pia waliotoka nje ya mji on
thanksgiving dinner mwaka Jana. Wale waliofika Kwangu watatoa ushahidi.
5. NIMEJITOLEA kufundisha darasa la Kiswahili
kwa watoto wa kitanzania hapa DMV. Darasa hili hukutana kanisani. Watoto wengi
wa Shule hii si waislamu na walimu wote si waislamu (I'm the only MUSLIM
teacher) na tumefanya kazi pamoja bila matatizo yeyote.
http://lukemusicfactory.blogspot.com/2013/04/darasa-la-kiswahili-leo-jumamosi-dmv.html?m=1
6. Nimeshiriki misa katika Makanisa tofauti,
nimepika na kusimama kuserve vyakula kwenye Matukio mbalimbali ya marafiki
zangu Kama ubarikio wa watoto wetu. Vipaimara na Misiba yaliyofanyika kanisani.
7. TAMCO ni umoja wa waumini wa Dini ya kiislamu
na Mimi ni mwanachama wa TAMCO na nipo kwenye Kamati ya uongozi. Nimeshirikiana
na waislamu wenzangu katika mambo ya Ibada kwani nimezaliwa na kulelewa katika
Imani ya Dini ya kiislamu na ninaipenda Dini yangu. Nimeshiriki katika
maandalizi ya sikukuu zote za kidini, Nimeshiriki katika maandalizi ya mfungo
wa Ramadhan na katika mambo yote yanayohusu Dini yetu na nimewakaribisha
marafiki zangu wasio waislam Kuja kushirikiana nasi katika sherehe zote za
kiislamu. TAMCO
imekaribisha watanzania wote bila kujali imani zao.
http://www.jestina-george.com/2014/07/libe-aungana-na-iftar-ya-tanzania.html
8. Nimehudumia jamii ya Wanawake wa
Kitanzania bila kujali Imani zao, sasa hivi ninaandikisha kila mwanamke wa
Kitanzania anayeishi hapa DMV kupata huduma ya bure ya mammogram na kampuni
moja hapa DC ambaye founder wake ninafahamiana naye na si muislamu, na tumeisha
anza kuweke mipango ya kwenda Tanzania next summer for medical mission trip
kutoa huduma ya matibabu na semina ya mambo tofauti yanayohusiana na afya.
Nimeshiriki katika makongamano ya wanawake na kila kitu kinachomhusu mwanamke
wa dini yoyote hapa DMV.
HITIMISHO:
Hayo yote yanayosemwa kuwa mimi ni
mbaguzi wa dini si ya kweli na vidhibiti hivyo hapo juu. Nimetumikia na
kujitolea elimu yangu, uzoefu na malezi niliyopata maishani katika kujenga
jumuiya yetu. Ushauri wangu kwa wagombea wa uongozi ni kuacha kuandika habari
zisizo na uhakika kuhusu wanajumuiya na kuwaharibia mahusiano na mtazamo wao
kwa jamii bali mjikite katika kutangaza mchango wako ulioutoa kwa wanajumuiya
au utakaoutoa kwa wanajumuiya. Hizi campaign ni za kuwa kiongozi wa kuhudumia
jamii bila kipato chochote. Tuonyeshe heshima na upendo baina yetu na si
kuandika mambo yanayohatarisha upendo na kuleta mpasuko kwenye jumuiya yetu.
Shukran,
Asha Nyang’anyi.
Kama una comment nitumie
ashany2@yahoo.com