
Kiungo mshambuliaji aliyechezea timu ya Chelsea ya Uingereza kwa miaka 13 amejiunga na ligi ya Major League Soccer ( MLS ) ya nchini Marekani na amesajiliwa na timu ya New York City FC.
Frank Lampard miaka 36 aliyehamia Chelsea mwaka 2001 kwa uhamisho wa pauni 11 kutoka West Ham ameweka rekodi kwenye club yake ya Chelsea kwa kuifungia magali 211 katika mechi 649 alizocheza.
Chelsea siku zote itakua moyoni mwangu nimekua na timu hiyo kwa miaka 13 nayoweza kuiita ya kujivunia lakini maisha lazima yaendelee ndio maana leo nipo na New York City FC, alisema Frank Lampard alipokua akiongea na waandishi wa habari.
Timu hii ya New York FC inamilikiwa na mmiliki wa Machester City ya Uingereza ambaye pia amemsajili mchezaji mwingine kutoka Spain, David Villa ambaye atakuwa kwa mkopo kwenye timu hii ya New York City FC kwa miezi 3 kuanzia October mpaka December 2014..
No comments:
Post a Comment