Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni na Terrence J. Jenkins, mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment (wa pili kulia) Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records (wa pili kushoto) na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wasanii nyota wa muziki na filamu kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitumia simu yake ya mkononi kuwaonesha vivutio vya kitalii wasanii nyota wa muziki na filamu wa Kimarekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania. Wasanii hao ni Terrence J. (Jenkins), mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment, mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group. Wengine ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wasanii nyota wa filamu na muziki kutoka Marekani walioko nchini kwa ziara ya kutoa mafunzo kwa wasanii wa Tanzania.
Picha ya pamoja.
PICHA NA IKULU
THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
|
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
Fax: 255-22-2113425
|
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMB O VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Jumatatu
Julai 14, 2014 amekutana na kundi la wasanii kutoka Marekani lililowasili
nchini usiku wa Alhamisi, Julai 10, 2014, kwa ajili ya kuendesha mafunzo kwa
wasanii wa Tanzania kwenye Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mjini Dar es
Salaam.
Wasanii
hao ni pamoja na Terrence J. (Jenkins),
mwendeshaji wa kipindi cha muziki kwenye televisheni ya E! Entertainment,
mwigizaji wa filamu na mtunzi wa vitabu na Revi Shelton, Mtendaji wa Shughuli
za Muziki katika Kampuni ya Outlet Media Group.
Wengine
ni Chaka Zulu, Mtendaji wa Shughuli za Muziki kutoka Kampuni ya Disturbing The
Peace Records na Davis Banner, mwigizaji, mwanamuziki, mtunzi na msimamizi wa
shughuli za muziki ambaye amepata kushinda tuzo maarufu ya Grammy.
Kiasi
cha wasanii 250 walishiriki semina hiyo inayoitwa Mafunzo ya Uendelezaji
Usanii. Hiyo ilikuwa ni kutimiza ahadi aliyotoa Rais Kikwete kwa wasanii wa
Tanzania kuwa atachangia kuinua kiwango cha ujuzi na weledi wao kwa kuwaandalia
mafunzo yatayoendeshwa na magwiji wa sanaa kutoka Marekani sasa imetimia.
Akizindua
Kampeni ya Uzalendo kwa Vijana inayoendeshwa na Muungano wa Wasanii Tanzania
kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma mwezi uliopita, Juni 14, 2014, Rais
Kikwete aliahidi kuchangia kuinua kiwango cha usanii na weledi wa wasanii wa
Tanzania kwa kusaidia kuandaa mafunzo yatakayoendeshwa na wasanii maarufu
kutoka Marekani.
Mbali
na kuendesha shughuli za mafunzo ya wasanii ambazo wamekuwa wakizifanya kwa
makundi madogo madogo tokea walipowasili nchini, pia wanamuziki hao wa Marekani
na kundi la wapiga picha watatembelea sehemu mbali mbali nchini, hasa kwenye vivutio vya watalii, ambako
watapiga picha na kuandaa vipindi vya kuitangaza Tanzania katika vyombo vya
habari vya Marekani.
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.
15 Julai,2014







1 comment:
kitu kimmoja napenda kumpa sifa yake raisi wetu na ambacho sidhani kama kutakuwa na raisi atafanya hivi ni kuwakaribisha watu kuja ikuluu na kuonana naye,this president is the best na ana roho nzuri kweli tafauti na maraisi waliopita waliko kuwa wanajifanya wao ndo wao kama mungu mtu.
Mungu akubariki sana jakaya kikwete.
kila binadamu ana mapungufu yake na mazuri yake na lazima apewe haki yake ya mazuri yake haya.
Post a Comment