Mbunge
wa Chalinze, mkoa wa Pwani, Mtoto wa Rais, Ridhiwani Kikwete, akijaribu
kimoja kati ya vitanda 267, kabla ya kuvigawa kwa shule saba za jimboni
Chalinze, katika hafla iliyofanyika jana, kwenye shule ya Sekondari
Lugoba jimboni humo. Shule zilizopewa vitanda hivyo vikiwa na magodoro
yake, idadi ya vitanda ilivyopata ikiwa kwenye mabano ni; Chalinze (50),
Moreto (50), Mandera (25), Talawanda (24), Kiwangawa (50), Lugoba (38)
na Kikaro (30). Kwa mujibu wa Ridhiwani mgawo huo ni wa awamu ya kwanza.
Ridhiwani
akimkabidhi vitanda 50 Mwalimu Emmanuel Kahabi kwa ajili ya shule ya
Chalinze. Kushono ni Abubakari Mlawa wa Kampuni ya MM Steel iliyotoa
vitanda hivyo
Abdalla Sakasa wa
Lugoba- akikabidhiwa vitanda vitanda 38
Charles Mussa wa Talawanda- vitanda 24
Omari Msami wa Kikaro-vitanda 30
Rose Umila wa Mandera Girls vitanda 25
Saidi Ally wa Kiwangwa akipongezwa na wadau baada ya kupata vitanda 50.
Ridhiwani akifurahi na wanafunzi wa shule ya Talawanda baada ya kukabidhi vitanda kwa mwalimu wa shyle hiyo (kulia)
Mgawo awamu ya kwanza
Ridhiwani
akizungumza na wadau kueleza mikakati mbalimbali ya kukwamua maendeleo
ya jimbo la Chalinze, ambapo alieleza kuwa miongoni mwa vipaumbele ni
huduma za umeme ambapo italetwa Transfoma itakayowezesha jimbo hilo
kupata umeme wa uhakika, afya na elimu
Wadau wakimsikiliza Ridhiwani. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO-CCM Blog
2 comments:
Tukaange kwa mafuta yetu Baba!!
This is what we want, msisahau kutoa vitanda wodi za kina mama jamani. Wazazi wanajifungua katika mazingira magumu sana.
Post a Comment