ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 7, 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AIWAKILISHA TANZANIA KATIKA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA UHURU WA MALAWI

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni Mama Asha Bilal.
 Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe, Malawi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika jana Jumapili.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili.
 Rais wa Malawi, Profesa. Arthur Peter Mutharika, akikagua gwaride wakati wa sherehe hizo.
 Askari wa Jeshi akisimamia na kuwapanga wananchi wasiingie uwanjani....
 Makundi mbalimbali pia yalijitokeza kuandaa sare na kuhudhuria sherehe hizo....
 Baadhi ya kinamama wakiwa katika sare ya Kitenge cha Mutarika...
 Vikosi vya usalama, vikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa pole na haraka.....
 Mwendo wa pole. Picha na OMR

No comments: