Ndugu Watanzania
Asubuhi ya leo tarehe 28 Julai 2014 nilitoa taarifa maalumu kwa vyombo vya habari nikiitaka Serikali kutolea ufafanuzi malalamiko yaliyojaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari. Asante Mungu kwamba Serikali imetolea majibu jambo hili kwa kusitiza ajira zote.
Rejea taarifa yangu kwa vyombo vya habari niliyoitaka Serikali kutoa majibu katika suala hili asubuhi ya leo tarehe 28 Julai na nakala yake kutumwa katika ofisi mbalimbali za Serikali.
Nachukua fursa hii kuipongeza Serikali kwa kuwa sikivu katika hili na huenda katika mengi yajayo, kama Rais Mtarajiwa wa Tucta baada ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 4-5 Dodoma, naahidi kushirikiana na Serikali hasa kama itakuwa sikivu.
Nahitaji kupatiwa majibu pia juu ya hatima ya mabaamedi wanaolazwa chumba kimoja zaidi ya kumi tena siyo katika vitanda, bali zaidi huwa wanalala chini; wanafanyakazi hadi usiku, wengine wanakoishi ni mbali na baa, hoteli nk.
Nahitaji kuona kero za walimu, wafanyakazi wa Serikali za Mitaa, madini, simu, kilimo, utafiti afya, mawasiliano, reli, bandari nk zinakomeshwa; Ni aibu hadi leo kuna walimu wanapoanza kazi wanalala kwa walimu wakuu wakisubiri kupatiwa sehemu za kuishi, ni aibu hadi leo mwalimu anafanyakazi kazi miezi sita inapita hakuna mshahara anaolipwa…hatuwezi kwenda hivi, ni lazima majibu yapatikane.
Wafanyakazi wa Tanzania tunapaswa kuimba nyimbo zingine, siyo za kero zile zile kila kukicha. Naamini yote yanawezekana, cha msingi ni kwa Serikali na waajiri kusimamia kwa haki mambo yote juu ya wafanyakazi. Hakuna lisilowezekana tukipigania haki.
Imetolewa leo Julai 28, 2014
na Dismas Lyassa
(Mgombea Uraisi TUCTA) 0754 49 8972/0712183282
na Dismas Lyassa
1 comment:
ndg Dismas nikupongeze, kwa ujumla serikali inabeba lawama zote, kwanini mambo madogo kama haya yanafumbiwa macho, hakuna haki Tanzania, kwanini watu wafanyakazi tena kwa malipo madogo wananyanyasika hivi?? Mfano mdogo tu kama huuwa mhudumu wa baa anahudumia watu wengi na wanaotumia fedha nyingi sana lakini hawapati hata ile TIP!! bado mshahara wao mdogo hawawezi enda nyumbani kwao kulala zaidi ya tano, wenye hizi baa nao wapewe majukumu!! yalotajwa mengi kweli yanahitaji ufumbuzi Bungeni tunakula fedha nyingi na bila kutoa huduma kwa wananchi na hata tukirejea kwenye majimbo ni hadithi tuuuu>>
Post a Comment