Advertisements

Thursday, July 17, 2014

TAMKO JUU YA TUHUMA ZA LIBERATUS MWANGOMBE KUHUSU DARASA LA KISWAHILI - TEAM IDDI SANDALY


Kwa masikitiko Makubwa nimesikitishwa na Mgombea Liberatus Mwangombe kulishutumu Darasa la kiswahili na kujaribu kuonyesha kuwa Darasa limekufa na hakukuwa na mipango ya kueleweka kwenye Darasa hili. Habari hizi ni za uongo, ubinafsi na hazijali Juhudi wala kuthamini Watanzania wana DMV waliojitolea.

Japo Mgombea huyu alianza kwa kusema kuwa hatojihusisha na negative campaign lakini kilichofuata ni kulishambulia Darasa na Mpango mzima wa Darasa hili.

Jumuiya tulianzisha Darasa hili kwa upendo na kuthamini  Nchi, lugha na Watoto wetu . Inasikitisha kuona baada ya kupongeza juhudi hizi za Jumuiya yetu Tukufu ya DMV. Mgombea aliamua kulishambulia Darasa hili na Kuwadhalilisha wale wote waliojitolea kwenye Darasa hili pamoja na Walimu.  Hali hii inakatisha tamaa na na sidhani kama ni Dalili nzuri .

Walimu na Viongozi wa Jumuiya tunategemea watanzania wote kuonyesha moyo wa shukrani kwa kazi kubwa tuliyoifanya kuifikisha shule hapa ilipo kwani matokeo yameonekana watoto wetu wanaongea kiswahili, wanajua hesabu kwa kiswahili , wanajua kuimba wimbo wa taifa. Na walimu ni wanachama wa vyama vya lugha ALTA, NCOTCL na wanatambulika katika mikutano hii kama walimu wa shule ya kiswahili wa Jumuiya ya DMV.

Mmoja ya Walimu Aliandaka na kusemakweli nimesikitika sana kusikia habari alizotoa Bwana Libe . Mimi ni mmojawapo wa walimu tulioanza kufundisha darasa hili kuanzia siku ya kwanza chini ya uongozi wa Jumuiya. Na tumefanya kazi usiku na mchana kuhakikisha madarasa haya yanafanikiwa. Kabla ya shule kuanza tulikaa chini tukatafakari na kutafuta msaada kwa wataalamu wa kiswahili toka vyuo mbali mbali na kupata muongozo wa jinsi gani shule hii itafanikiwa. Mojawapo ya mambo yaliyokuwepo ni kupanga malengo ya shule yetu, kupata elimu na kuwa na syllabus ya mwaka mzima. Na kwa taarifa tu haya yote TULIYATEKELEZA kabla ya kufungua shule except kwenda kusoma ilibidi tusubiri summer time wakati kozi hizo zinatolewa. Tuna documents tulizoziandika za kueleza malengo yetu, na sisi walimu watatu tuliamua kwenda kusoma Indiana na kupata cheti kama foreign language teachers for swahili hapa Marekani na tunafanya kazi kwa karibu sana na Maprofessor wa kiswahili hapa Marekani na darasa hili linatambulika kwa kila mwalimu anayefundisha kiswahili almost all colleges over USA. Tumeshiriki mikutano ya lugha kwa gharama zetu ili kutimiza malengo tuliyojiwekea ya kuiendeleza hii shule yetu. Na tumekwishafanya mazungumzo na walimu wa kiswahili wenye summer program ili waweze kuwachukua watoto kutoka katika madarasa yetu ya kiswahili ili tuanze kuwatayarisha for future professions in Swahili. Najua tupo kwenye campaign but ningeomba kabla ya kutoa habari nzito kama hii mgombea LIberatus angewasiliana nasi tumueleze kwa nini darasa limesimama.  Tumeweza kufanya yote haya from our own funds from our own salary or any source of income, kulipa nauli, membership fees za organizations na nauli za kusafiri kwenda kusoma au conference so we take everything very serious that's why i thought i need to put this details out here”

Sababu Ya Darasa kusimama ni: darasa hili lilikuwa likiendeshwa kanisani, kanisa ambalo katibu ni muumini na akatumia uhusiano wake na uongozi na tukapata madarasa ya bure. Baada ya mkataba kuisha na sisi kama shule tukawa affected sababu tulitulimia venue hii kufundisha kiswahili kwa mgongo wa kanisa.

Hivi Sasa Mipango ya Darasa Kuanza imekamilika na Tunawangoja watoto waendelee na Likizo ya Summer ambayo inaendelea Mashuleni na Venues zimepatika na Jumuiya na Ubalozi wetu wa hapa Washington DC tuko katika hatua za Mwisho za kuweza kukamilisha mikataba ya  Permanent Location kwa Darasa letu la Kiswahili.

Darasa lipo, Linaendelea na DMV Inazidikuendelea na kuwa mfano kwa Jumuiya nyingine.

Mungu Ibariki DMV

Wenu
Iddi Sandaly

DMV KWANZA