Na Mwandishi wetu, New York.
Uchaguzi wa viongozi wa DMV hua kivutio kwa majimbo mengine na nje ya Marekani kwa wengi kujiuliza kuna kitu gani wanachopigania na wengine kudiliki kusema utafikiri wameahidiwa kufanyakazi na Rais Obama.Vijimambo imeongea na watu mbalimbali kutoka majimbo tofauti, Canada, Uingereza na Tanzania na watu wengi wameonekana kufuatilia chaguzi za DMV kwa karibu zaidi kutokana na wagombea wake kujinadi kwa staili ya aina yake mpaka imepelekea Watanzania wanaoishi majimbo ya karibu na DMV wanafikiria kuja siku ya uchaguzi kushuhudia aina ya uchaguzi huu utakavyokua.
Vijimambo ikiongea na Salim Akida wa New York, amesema
kusema ukweli uchaguzi wa DMV ni wa next level kwa sababu tangia aje nchini Marekani na hata huko alikotoka hajawahi kuona uchaguzi uliokua moto namna ya DMV na kila siku naingia kwenye mitandao kufuatilia leo mgombea kasema nini.Kkusema ukweli tunaufuatilia uchaguzi wa DMV kwa karibu sana na siku ya uchaguzi nitakuwepo DMV kushuhudia uchaguzi huu.
Vijimambo iliongea na Andrew Madeje wa Kansas amesema yeye anaufuatilia uchaguzi huu kwa karibu sana pia wagombe wa Urais ni marafiki zangu facebook mpaka hua najiuliza kunanini kwenye Jumuiya hii ya DMV mbona moto ni mkali sana katika kujinadi, kusema ukweli Vijimambo kwa jinsi uchaguzi unavyokwenda nategemea DMV itapata viongozi wazuri.
Pia Vijimambo iliongea na Jimmy Kilauli ambaye kwa sasa yupo nchini Uingereza kuhudhuria Maafali ya mtoto wake amesema tangia Tanzania ninaufuatilia kwa karibu uchaguzi huu wa DMV kusema ukweli ni uchaguzi wa kipekee nachoomba baada ya uchaguzi wawe kitu kimoja walioshinda na watakaoshindwa waache tofauti zao na wafanyekazi kama WanaDMV. Nafikiri ni vizuri kuwa na chaguzi za aina hii kwa ajili ya kutafuta kiongozi wa kweli.
Chaguzi za DMV zilianza kubadilika miaka miwili iliyopita kwa wagombea wakati huo Bi. Lovenes Mamuya na mgombea anayegombea sasa hivi kwa mara ya pili, Bwn. Iddi Sandaly kwa kuweza kujinadi kwa Watanzania DMV kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo Video na kutengeneza vipeperushi vyenye picha zao vilivyowekwa kwenye kurasa zao za facebook na mitandao mingine.
Chaguzi ya mwaka huu umekuatofauti kidogo watu wengi hasa wafuasi wa wagombea wamekuwa karibu sana na wagombea wao bila kificho na wengine wakiweka kura zao wazi kwenye mitandao ya jamii ya mgombea gani atakayempigia kura. Kitu kingine kilichojitokeza mwaka huu ni Balozi wa Tanzania Mhe. Liberata Mulamula kuwaita wagombea wote wakiwemo kamati ya uchaguzi na kuweza kukaa nao chini na kuongea nao kwa kina kuhusiana na uchaguzi huu uliopangwa kufanyika Aug 9, 2014.
Timu ya Vijimambo inawatakia kheri na baraka wagombea wote hata kama siku ya uchaguzi hautachaguliwa wewe ujione ni mshindi kwa WanaDMV na viongozi waliochaguliwa bado wanahitaji ushirikiano wako. Tunaomba uchaguzi uwe wa amani na utulivu kusudi uwe mfano wa kuigwa kokote ulimwenguni na kwa Pamoja DMV Tunaweza.
2 comments:
Kamati ya uchaguzi tafadhali tunahitaji midahalo mitatu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati kabisa Wagombea uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio DMV, Wajumbe wa Bodi na Tume ya Uchaguzi kwa heshima mliyonipa kukutana nanyi na kwa mazungumzo mazuri tuliyofanya.
Aidna napenda kuwapongeza wale wote waliojitokeza kugomba nafasi mbali mbali za uongozi na kuungana na Vijimambo kuwatakia heri na baraka katika uchaguzi huo.
Rai yangu kwa Watanzania wenzangu wana DMV ni kwamba mjitokeze kwa wingi kujiandikisha kabla ya tarehe 7 August 2014, tarehe ya mwisho ya kujiandikisha na hatimaye na hatimaye kushiriki kwenye uchaguzi na kupiga kura tarehe 9 August 2014. Aidha naipongeza Tume ya Uchaguzi kujitolea kusimamia uchaguzi huu pamoja na chanagmoto zote chini ya uongozi wa Bodi.
Ninaomba pia kama wengine wote tuwe na uchaguzi ulio tulivu,huru na haki. Aidha ni mtarajio na imani yangu kuwa baada ya uchaguzi wagombea wote watakuwa kitu kimoja katika kuunga mkono viongozi watakaochaguliwa katika kudumisha na kuimarisha umoja, upendo,amani na mshikamano wa wana Jumuiya wote.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Wabariki Wanajumuiya ya DMV na Watanzania wote popote walipo.
Wenu,
Balozi Liberata Mulamula
Ubalozi wa Tanzania
Washington DC.
Post a Comment