Mfanyabiashara wa maduka ya nyama wa Ipagala, Naomi Peter, alithibitisha kuwapo tatizo hilo na kuongeza kuwa wengine wanatumia hata vichwani, kitendo ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na walaji.
Mwenyekiti wa Soko Kuu la Majengo, Godson Rugazama, pia alithibitisha kuwapo tatizo hilo na kusema lipo kwa manispaa nzima.
“Wanabeba nyama mabegani, ingawa wanafahamu kuwa ni makosa kiafya.
Pamoja na kutumia gari maalumu ya kusafirishia nyama, hawana vifaa kwa ajili ya kulinda usalama wa afya zao na walaji,” alisema Ragazama.
Mmoja wa walaji, Chadulu Kisanga, alisema tabia hiyo inatishia usalama wa afya zao na kwamba, ikiwa yanafanyika mbele yao wanashindwa kuelewa inavyopakiwa kwenye magari.
“Bora uwekwe utaratibu wa nyama kupakiwa kwenye makasha, ambayo usafi wake utahakikiwa na maofisa wa afya. Ndipo yawekwe kwenye gari ili wanaopakia na kupakua washike makasha wakati wa kupakia na kupakua,” alishauri Kisanga.
Mwajuma Hassani, ambaye ni mkazi wa Chang’ombe, alisema huwa anakutana na watu wakiwa wamebeba nyama mabegani, wakiitoa kwenye gari na kuiingiza buchani, huku na sare zao zikiwa zimelowa damu na nyingine usafi wake ukiwa hauridhishi.
Aliomba mamlaka zinazohusika kuhakikisha mtindo huo wa ubebaji unakomeshwa kwa kutafutwa njia mbadala ili kutunza staha ya chakula hicho na afya za watu.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Augustine Kalinga, aliahidi kufanyia kazi malalamiko hayo akieleza kuwa hawezi kuyazungumzia kwa kuwa bado ni mgeni.
CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment